Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia auwawa na mbwa wake

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia auwawa na mbwa wake

Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia Chipolopolo, Philemon Mulala ameuawa na mbwa wake nchini Afrika Kusini.

Msemaji wa polisi, Sam Tselanyane, alisema kuwa mke wake aliwaambia kwamba alisikia mbwa wakibweka lakini hakujishughulisha na kwenda kuangalia ni nini kilikuwa kibaya kwani mbwa hao mara kwa mara walikuwa wakiwabwekea watembea kwa miguu na magari yaliyokuwa yakipita.

“Baada ya umeme kurudi, niliingia ndani kumtafuta mume wangu lakini sikumpata. Niliendelea na upekuzi kisha nikamuona akiwa amelala nje kwenye bustani. Nilipotoka nje kupeleleza kulikoni, nikagundua mume wangu alikuwa hatikisiki baada ya kuumwa na mbwa wetu watatu,” alisema mke wa Mulala.

“Nilipiga ripoti kwa polisi na kuomba msaada wa kumpeleka hospitalini ,lakini walipofika walisema ameshafariki.”

Aidha mamlaka zimewaondoa mbwa hao wawili ambao ni 'Cross breed" ya Pitbull na mbwa wa tatu hajulikani asili yake ila anasemekana kuwa mkali.

Mulala alihamia Afrika Kusini kuichezea klabu ya Kaizer Chiefs mwaka wa 1988. Pia alichezea Cape Town Spurs na Lenasia Dynamos kabla ya kustaafu.

Shirikisho la soka la Zambia (FAZ) limetoa taarifa ya kuomboleza kifo cha Mulala likisema alikuwa sehemu ya kikosi cha Zambia cha mwaka 1984 kilichoshinda Kombe la East and Central Africa Challenge.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags