Mbunge nchini Kenya afariki kwa ajali ya pikipiki

Mbunge nchini Kenya afariki kwa ajali ya pikipiki

Mbunge kutoka nchini Kenya, Kullow Hassan Maalim, amefariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu hospitalini baada ya kuhusika katika ajali ya pikipiki iliyomgonga na kukimbia, katika mji mkuu wa Nairobi.

Kullow alikuwa mbunge wa awamu ya pili wa eneo bunge la Banisa kaskazini-mashariki mwa Kenya.

Familia ilithibitisha hilo kupitia vyombo vya habari na kueleza kuwa mbunge huyo aligongwa Jumamosi na mhudumu wa teksi ya pikipiki aliyekuwa akiendesha kwa kasi na kupelekea kufariki siku ya Jumanne usiku.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags