Mbosso, Yammi  kama  Shah Rukh Khan na Kajol

Mbosso, Yammi kama Shah Rukh Khan na Kajol

Wanamuziki wa Bongo Fleva nchini Mbosso na Yammi wamejifananisha kama waigizaji kutoka nchini India Shah Rukh Khan na Kajol, hii ni baada ya kuachia video wakiwa chooni.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Mbosso ame-share video akiwa na #Yammi ikiambatana na ujumbe usemao ‘Sharukhan & Kajol’ huku ikisikika sauti ya Mbosso katika wimbo wa ‘Ni Busu’ wa Barnaba aliyomshirikisha Yammi.

Imeelezwa kuwa #Yammi, Mbosso na #Barnaba tayari wameshafanya remix ya ngoma hiyo iliyotoka mwezi mmoja uliyopita huku video yake ikiwa na zaidi ya watazamaji Elfu Sabini.

Katika video hiyo iliyopostiwa na #Mbosso baadhi ya wasanii wamejitokea katika upande wa ‘koment’ wakimtania Mbosso akiwemo #Zuchu ambapo aliandika ‘Wifi’ ikiambatana na emoji za upendo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags