Mavoko kwenye kwato za Nature

Mavoko kwenye kwato za Nature

Namwona Rich Mavoko kwenye kwato za Juma Nature. Siyo kwamba kabadilika kila kitu, hapana ni yuleyule lakini mapokezi ya ngoma zake siyo kama Rich Mavoko wa WCB.

Na kitu kimojawapo ni mazingira yanaonesha Rich Mavoko anategemea zaidi kipaji kuliko fujo za kiki nje ya kipaji chake. Kitu ambacho kilifanya pale WCB aonekane Diamond kwanza kisha Harmonize. Baadaye mashabiki wajichagulie anayefuata kati ya Mavoko na Rayvanny.

Siyo kwa uwezo wa kuimba na kutunga mashairi, hapana, kwa maana alitajwa zaidi Diamond mwenyewe kwenye vinywa vya watu kutokana na aina ya maisha yake, kisha Harmonize. Hawa jamaa mbali ya muziki wana fujo nyingi za maisha ya mapenzi.
Hiki kitu kilimshinda Mavoko akasimamia muziki wake tu.

Yote kwa yote hadi sasa sijamuona Rich Mavoko wa Show Me, aliyemfanya Harmonize atamani ngoma isitoke ili atengeneze ‘verse’ tamu zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags