Whozu atemana na Too Much Money

Whozu atemana na Too Much Money

Msanii Whozu amejitoa kwenye record label ya Too Much Money na sasa ni msanii anayejitegemea.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Whozu ameweka taarifa rasmi ya kuondoka kwenye lebo hiyo huku akiwashukuru uongozi huo kwa kumsimamia kwa muda wote ambao wamefanya kazi kwa pamoja.

“TOO MUCH MONEY kwangu itabaki kuwa familia ya kudumu na nitashirikiana nao nyakati zote ushirikiano utakapohitajika. Hivyo kwa maneno haya machache namaanisha kuwa kwa sasa WHOZU hayupo tena chini ya TOO MUCH MONEY. Asanteni TOO MUCH MONEY kwa kuniamini na kuniaminisha kwa Watanzania, sisi ni familia” ameandika Whozu.

Whozu alisaini mkataba Novemba 6, 2019 na kampuni ya entertaint ya Too Much Money inayoongozwa na kaka yake Frank Knows pamoja na Fred Vunja Bei yenye ofisi zake jijini Guangzhou, China.

Mkataba huo ulihusisha kusimamia kazi za muziki, vichekesho pamoja na biashara ambazo zitahusisha jina la msanii huyo, mkataba huo mrefu ambao kwa mujibu wake alilipwa Dola za kimarekani 30,000 kama Deposit ambazo ni zaidi ya Millioni 60 za kibongo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags