Mashabiki wa Card B waivaa vita ya Megani, Nick Minaj

Mashabiki wa Card B waivaa vita ya Megani, Nick Minaj

Baada ya mashabiki wa Nicki Minaj kutaja sehemu aliyozikwa mama mzazi wa ‘rapa’ Megan Thee Stallion, na kutishia kwenda kufukua kaburi hilo, na sasa mashabiki wa #CardiB waingilia kati bifu hilo kwa kutaja sehemu ambayo amezikwa baba mzazi wa #Nicki.

Mashabiki hao ambao wanatambulika kama ‘Cardi Gang’ wameamua kukinukisha kupitia mtandao wa X ambapo walitaja sehemu alipozikwa Baba Nicki huko Utica, New York 13501.

Ikumbukwe kuwa siku ya juzi Januari 31, polisi nchini Marekani waliongeza ulinzi katika kaburi la mama Megan (Holly Thomas) baada ya mashabiki hao kutaka kufukua kaburi hilo.

Megan na Nicki wameingia katika bifu zito baada ya Megani kuachia ngoma ya ‘Hiss’ iliyodaiwa kumchana mume wa Nicki ‘Kenneth Petty’ na kisha Nicki aliamua kumjibu kwa ngoma ya ‘Big Footy’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags