Marioo: Turekebishe Iphone Users au tutoe nyingine

Marioo: Turekebishe Iphone Users au tutoe nyingine

Baada ya sakata lake na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kukamilika mwanamuziki Mario amewauliza swali mashabiki kama waurekebishe wimbo wa ‘Iphone Users’ au atoe ngoma nyingine.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Marioo ame-share video akiwa anaimba wimbo huo huku ukiambatana na swali ‘Turekebishe huu wimbo kama Inavyotakiwa au Tutoe Machine Nyengine?.

Utakumbuka kuwa wiki iliyoisha Marioo alishare taarifa kwenye instastori yake akidai kuwa hajafanya promotion ya wimbo wake wa ‘Iphone Users’ kwa sababu Basata wamemwambia kuwa wimbo huo haujazingatia maadili.

Hata hivyo baada ya kuweka wazi suala hilo siku mbili zilizopita Marioo aliitwa na Basata kwa ajili ya majadiliano na Katibu Mtendaji wa Basata Dkt. Kedmon Mapana ambapo Katibu alimkabidhi mwongozo wa maadili katika kazi za Sanaa Marioo huku akimtaka akafanye marekebisho katika wimbo wake wa “Iphone user”.

Marioo aliuachia wimbo huo wa ‘Iphone Users’ wiki mbili zilizopita ambapo mpaka kufikia sasa unazaidi ya watazamaji 469,135 katika mtandao wa YouTube.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags