Marekani yazidiwa na wahamiaji

Marekani yazidiwa na wahamiaji

Kufatiwa sehemu za makazi ya kuwahifadhi wahamiaji katika jiji la Texas nchini Marekani imeeleza kuwa imezidiwa uwezo kutokana na wimbi kubwa la wahamiaji nchini humo.

Wahamiaji hao wengi waliofika katika mji wa Brownsville kusini mwa Texas wamepelekea watoa huduma za kijamii kuelemewa na kusababisha kukataliwa baadhi ya wahamiaji katika sehemu za kuwasaidia watu hao.

Huku mamia ya wahamiaji kutoka Mexico kuwapa kazi ngumu maafisa wa Marekani kuhudumia makundi makubwa ya watu wanaokimbia umaskini na vurugu kwenye nchi zao.

Maafisa wanaeleza kuwa  zaidi ya wahamiaji 15,000, wengi wao kutoka Venezuela, wiki iliyopita walivuka mto ulio karibu na mji huo wa Brownsville kinyume cha sheria hali ambayo imeogeza wahamiaji kuwa wengi.

Aidha maafisa wa ulinzi wa mipaka katika jimbo la Texas wamesema hilo ni ongezeko kubwa la wahamiaji ukilinganisha na watu 1,700 walioingia kwenye eneo hilo hivi karibuni.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags