Mambo ya kuzingatia kwa wanachuo

Mambo ya kuzingatia kwa wanachuo

Oohoooo! Wanachuo kama likizo inaisha hivi au bado, vipi kwa upande wake GPA inasoma ngapi au tukuache kidogo sio shida zako, basi hayaa, leo kwenye UniCorner tumekusogezea mada konki ambayo itakusaidia wewe first year na wale ambao wanaokwenda kuendelea ama kumaliza mwaka wao wa masomo kupata matokeo mazuri.

Kama tunavyojua wanasema mwaka mpya na mambo mapya, ila usipobadilika kwelikweli mwaka huu utakuwa na mambo yale yale kama miaka mingine iliopita ukiwa chuoni.

Anyway, sitaki kukuchosha sana msomaji wangu ukiwa chuo haya ni malengo kadhaa unayoweza kujipangia ili usije kumaliza mwaka wako wa masomo vibaya.

  • Malengo ya kiuchumi

Jambo la kwanza la kuzingatia ni malengo ya hali yako ya kiuchumi jinsi ya kuweka bajeti na kuweka akiba. Cha kukushauri ukiwa chuo, ishi maisha yako yaani ishi maisha ya kwenu, maana kupretend maisha kutakualibia bajeti yako na uchumi wako kwa ujumla. Ikiwezekana kwa uchumi wako huo huo mdogo anzisha hata biashara ya hereni wauzie wanafunzi wenzako.

  • Malengo ya kitaaluma

Haya sasa hapa ndo kwenye balaa lenyewe, jambo jingine la kuzingatia ni malengo yako katika masomo yako, wewe mwenyewe ndo utapanga unataka GPA ipi na kuepukana na supp. Jiwekee malengo na ratiba ya kujisomea na kufanya kazi zote ambazo utakazo achiwa ili kuepukana na kupata wastani mdogo.

  • Malengo binafsi

Hapa ndipo penyewe sasa. Kwenye malengo binafsi hapa nitazungumzia kuhusiana na mahusiano yako. Sawa tunakujua kuwa umekuwa na unahitaji mtu wa kubadilishana nae mawazo, nikushauri tu kama ulikuwa na mahusiano yako kabla basi endelea nayo hayo hayo usihadaike na wanawake/wanaume wapya utakaokutana nao darasani.

Baki na msimamo wako na malengo yako, tamaa isikuponze wala usikubali mtu yoyote kukushawishi ujinga.

  • Malengo ya kiafya

Jambo la mwisho la muhimu ni kuzingatia afya yako kwa kula mlo kamili, kufanya mazoezi na jitahidi sana kuepukana na strees zisizo za lazima maana zinaweza kukutoka katika mstari wa kufikiria kilichokupeleka chuoni. Jali afya yako, achana na stress zisizo na msingi kuna mambo huwezi kuyaforce kwa uwezo wako, ukiona umezidiwa sana basi kwa dini yako muombe Mungu wako atakusaidia.

Cha kumalizia malengo hayatimii kwasababu umeyaweka, malengo yanatimia kwa vile unayafanyia kazi, hivyo jitahidi kuandika pia ni jinsi gani utayafanyia kazi ili yatimie, hatua utakazochukua na tabia utakazotakiwa kuwa nazo ili kutimiza malengo yako.

Haya wale wadau na wanachuo pitia mada hii ili uweze kujifunza zaidi na usisahau kufuatilia mitandao yetu ya kijamii @Mwananchiscoop, wacha niwaache na swali wanachuo, Je una malengo gani katika mwaka wako wa masomo? Dondosha komenti yako kwenye tovuti yetu.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post