Hello, I hope mko good kabisa. Leo katika biashara tunakuletea mawili watatu ambayo unatakiwa kuzingatia katika bishara yako. Kama tunavyoelewa, kipindi hichi ndo kipindi cha watu wengi kuzunguka katika maofisi na kutafuta kazi, wengine kutaka kuanzisha biashara kutokana na wanafunzi wa takribani vyuo vyote kumaliza masomo yao na kuwa jobless rasmi.
Sasa hapa leo tunazungumza na wale ambao wako na mpango wa kujiajiri na sio kuajiriwa, basi tutakujuza mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuanziasha biashara yako. Uzuri wa kazi yoyote katika biashara unategemea na umakini wa mfanyabishara katika kuzingatia mambo muhimu yenye kutoa mwongozo wa kibiashara.
Ni hekima kwa mfanyabiashara kujifunza mambo hayo muhimu kabla ya kuingia katika biashara, swala la msingi zaidi analopaswa kufahamu mfanyabiashara ni kwamba kuna mambo mengi katika biashara hivyo anaweza kujifunza moja baada ya jingine huku akiweka katika matendo kile anachojifunza, mfano anaweza kujifunza maswala ya masoko, usimamizi wa biashara, usimamizi wa miradi nk.
Mambo ya kuzingatia kwenye biashara yako
- Je bidhaa yako ni ya msimu au la?
Kila mfanyabishara anapaswa kujua aina ya bidhaa anayozalisha kama je ina soko la kudumu au ni bidhaa ya msimu tu. Kupitia kujua aina ya soko la bidhaa zake itamsaidia kujua ni kiwango gani anapaswa kuzalisha au kununua na kisha kwenda kuuza kwenye soko husika.
- Washindani wako ni kina nani?
Washindani wako ni makampuni au watu wanaozalisha bidhaa zinazofanana na za kwako. Ukijua washindani wako itakusaidia kuzalisha bidhaa zenye ubora na utofauti ukilinganisha na wao, hivyo utakuwa na uhakika wa soko la bidhaa zako.
- Unazalisha bidhaa zako kwa ajili ya nani?
Hili ni swali la msingi ambalo mfanyabiashara yoyote anapaswa kujiuliza kabla ya kuanza kutengeneza bidhaa zake. Kuna utofauti mkubwa kati ya utengenezaji wa bidhaa kulingana na umri, utamaduni wa watu fulani,taaluma ya watu fulani, mila na desturi za watu fulani.
Wakati mwingine pia kulingana na hali ya kijiografia ya eneo husika itakuwa jambo la ajabu kama mjasiriamali ataamua kutengeneza makoti mazito na masweta wakati anategemea wateja wake wanapatikana katika ukanda wa joto, ni vyema mfanyabiashara akajua vyema aina ya kundi katika jamii ambalo amekusudia kuliuzia bidhaa zake.
- Upatikanaji wa malighafi ukoje?
Malighafi ni vitu vyote ambavyo vinasaidia katika utengenezaji wa bidhaa, mfano kama wewe una mgahawa basi malighafi yako ni chumvi, sukari, mchele nk. Kujua upatikanaji wa malighafi kutakusaidia kujua ni wapi ufungue kituo chako cha biashara, itakusaidia kujua upange bei gani kulingana na gharama ya upatikanaji wa malighafi zako.
- Utahitaji kufanya matangazo ya biashara yako.
Ulimwengu wa sasa ni ulimwengu wa kidigitali na kumekuwa na matumizi makubwa ya teknolojia ya habari na wasaliliano, hivyo ni vyema ukajua njia sahihi ya kutangaza biashara yako.
Kuna utofauti mkubwa wa kutangaza biashara kwenye redio, televisheni, majarida, vipeperushi, mabango na hata katika tovuti. Mfano, matangazo ya kwenye mitandao ya kijamii yanapaswa kuwa na ujumbe wa moja kwa moja na mvuto wa picha wa hali ya juu kiasi kwamba, tangazo hilo litakamata akili ya anayeperuzi kwa urahisi ili aendelee kusoma na kuliangalia tangazo hilo.
Haya sasa wale wadau wangu wa Mwananchi Scoop ambao mna mpango wa kuanzisha biashara hivi karibuni basi kwa kusoma makala hii utaweza kupata uelewa kuhusiana na kipi ufanye ili biashara yako iweze kutambulika.
Leave a Reply