Mama yake Hakimi afunguka sakata la talaka ya mwanae

Mama yake Hakimi afunguka sakata la talaka ya mwanae

Baada ya sakata lililoshika vichwa vya habari duniani na kutrendi kupitia mitandao ya kijamii kuhusiana na mchezaji wa timu ya taifa ya Morocco na klabu ya PSG Achraf Hakimi kumuandikisha utajiri wake wote mama yake mzazi jambo ambalo lilimshangaza mkewe Hiba na mahakama kwa ujumla.

Basi bwana kupitia mahojiano na moja ya chombo cha habari nchini humo mama mzazi wa Achraf Hakimi, Saida Mouh amesema alikua hajui swala lolote kuusu maswala ya pesa na mali za mwanae na kwamba alikua amemficha kuusu jambo hilo kabisa.

Bi Saida alisema ni swala zuri kama mtoto wake aliamua kujilinda, amesema kama mtoto wake asimgechukua hatua hiyo kamwe asingeweza kutoka salama kwa aliyekua mke wake Hiba Abouk, mama Hakimi alimaliza kwakusema haoni tatizo kwa alichofanya mtoto wake na anajivunia mwanae kuchukua uamuzi huo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags