Madhara ya unywaji wa maziwa kwa wanaume

Madhara ya unywaji wa maziwa kwa wanaume

Mmmmmmmh! Sasa hivi inabidi kabla hatujala vyakula vyovyote tufuatilie na kuuliza vina madhara gani maana sio powa kila siku hali inazidi kuwa mbaya, ungana name kusoma Makala hii kuhusiana na madhara ya unywaji wa maziwa kwa wanaume.

Wanaume wanaotumia bidhaa za wanyama mara kwa mara, haswa maziwa, wana hatari kubwa ya asilimia 60 ya kupata saratani ya kibofu kuliko wale ambao hawatumii, kulingana na utafiti mpya.

Utafiti huu, uliochapishwa katika Jarida la Marekani la Lishe, ulifanywa na watafiti katika Chuo Kikuu cha Loma Linda, ambao walikuwa na nia ya kuchunguza uhusiano kati ya chakula na saratani ya kibofu.

Tangu 2001, watafiti wamekuwa wakifuatilia afya ya wanaume nchini Marekani na Canada.

 

Utafiti huo uliangalia lishe ya wanaume hao kwa miaka mitano

Baadhi ya wanaume hao waligunduliwa kuwa na saratani ya kibofu cha mkojo, na utafiti huo uliwalinganisha wale ambao hawakutumia bidhaa za wanyama na wale waliotumia.

Watafiti hao waligundua kuwa ulaji wa kalsiamu kutoka kwa vyanzo visivyo vya wanyama haukuwa na athari kwa hatari ya saratani ya kibofu cha mkojo.

 

‘’Matokeo yetu yanatoa ushahidi zaidi wa uhusiano kati ya bidhaa zitokanazo na wanyama na saratani ya kibofu,’’ alisema Gary Fraser, ambaye aliongoza utafiti huo.


Homoni za maziwa ya wanyama na saratani ya kibofu

Fraser alisema sababu moja ya uhusiano kati ya maziwa ya wanyama na saratani ya kibofu cha mkojo ni kwamba ugonjwa huo unajibu kwa homoni.

 Kwa ngombe wa maziwa wajawazito, homoni katika maziwa inaweza kuongeza hatari ya saratani ya kibofu.

Utafiti huo pia uligundua kuwa tafiti za awali zimehusisha unywaji wa maziwa na bidhaa nyingine za wanyama na kuongezeka kwa sukari kwenye damu, ambayo inadhaniwa kusababisha aina fulani za saratani. 

Matokeo ya utafiti huu ni sawa na yale ya utafiti mwingine uliofanyika mwaka 2020 ambapo watafiti walisema kuwa wanawake wanaokunywa maziwa ya wanyama mara kwa mara wako katika hatari ya kupata saratani ya matiti.

 

  Vyakula vitokanavyo na mimea 

Kinyume chake, tafiti nyingi zimegundua kuwa lishe inayotokana na mimea ni kinga dhidi ya aina fulani za saratani, pamoja na saratani ya kibofu.

Utafiti uliochapishwa mwaka jana katika Jarida la Urology ulifuatilia afya ya wanaume 47,243 katika kipindi cha miaka 28.

Lishe inayotokana na mimea inasemekana kupunguza hatari ya saratani ya kibofu.

 

Saratani ya kibofu ni nini?

  • Ni aina ya saratani inayojulikana zaidi kwa wanaume nchini Uingereza - jamii inayozeeka inamaanisha kuwa wanaume wengi wanaugua ugonjwa huo na wanafariki kutokana nao.
  • Hutokea kwenye kibofu cha mkojo kwa wanaume.
  • Saratani hii huweza kusambaa taratibu kwa miaka mingi na wanaume wengi huwa hawaoni dalili.
  • Dalili ni pamoja na kutoa mkojo mwingi na kuutoa kwa unyonge.
  • Hakuna kipimo kimoja cha kutambua saratani hii - vipimo vya damu na kimwili vinatumika katika uchunguzi.

Chanzo BBC







Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post