Kutokana hilo mashabiki na wadau mbalimbali wa muziki wake, wamekuwa wakizua mijadala mbalimbali na kuhoji jambo hilo huku wengi wao wakidai msanii huyo hatendewi haki.

Hata hivyo licha ya mijadala hiyo ipo mitazao inayoeleza sababu za msanii huyo kutoambulia tuzo.
Maudhui ya Muziki wa Tupac
Moja ya jambo ambalo limekuwa likizungumzwa kwa muda mrefu ambalo linadaiwa kumkosesha tuzo hizo msanii huyo ni maudhui ya muziki wake ambapo alikuwa akiimba nyimbo zenye maudhui ya kijamii, kisiasa, na kiuhalifu. Jambo ambalo lilikosa nafasi Grammy kutokana na waandaji wa tuzo hizo kuthamini nyimbo zenye maudhui ya upendo au mafanikio katika jamii.
Kukua kwa muziki wa Hip-Hop
Mwanzoni mwa mwaka 1990 muziki wa Hip Hop haukuchukuliwa kama chachu inayoweza kupendwa na kukabidhiwa Grammy hadi pale ilipoanza kutiliwa maanani miaka ya 2000.
Hii ina maana kwamba wakati 2Pac alipokuwa akifanya jitihada kubwa katika Hip Hop, muziki huo haukuwa na nafasi kubwa katika tuzo hizo na badala yake nyimbo ambazo zilipendelewa zaidi zikiwa ni za pop au rock.
Mashindano na wasanii wengine
Mbali na kuwa bora lakini pia msanii huyo anatajwa kuwa alikuwa akipenda kushindana na nyota wa kubwa ambao walikuwa na nafasi katika tuzo za Grammy akiwemo The Notorious B.I.G., Dr. Dre, na Snoop Dogg.
Kwa mujibu wa baadhi ya wadau wanadai kuwa msanii huyo alitakuwa kuwa mpole na kufuata nyendo za nyota hao ili kufanikiwa zaidi, hata hivyo jambo lingine lililofanya waandaji wa tuzo kumkwepa ni kutokana na matatizo ya kisheria ambayo yalikuwa yakimuandama.
Tupac kuchaguliwa kuwani tuzo za Grammy
Licha ya kutoondoka na tuzo hata moja aliwahi kuchaguliwa miaka ya nyuma katika vipengele kama Best Rap Solo Performance na Best Rap Album kupitia album zake ikiwemo All Eyez on Me na Me Against the World.
Ikumbukwe Tupac alizaliwa 16 Juni 1971 na alifariki dunia Septemba 13, 1996 baada ya kupigwa risasi Septemba 7, 1996 Las Vegas, Nevada alipokuwa ndani ya gari na mwenyekiti wa Death Row Records, Suge Knight.
Leave a Reply