Kuwa mwanafunzi wa chuo kunamaanisha nini kwako

Kuwa mwanafunzi wa chuo kunamaanisha nini kwako

Ooooyeeeeeh! It’s another Sunday, kama nawaona wanangu wa kula bata mshajipanga mnaenda kukidibua wapi hahahah! ni time ya kupotea kama soksi moja. Haya tuachane na hayo wanafunzi wote wa vyuo vikuu na vya kawaida, nina ujumbe wenu hapa leo hii.

Kuna wanafunzi wengi mpaka sasa ukimuuliza umekuja chuo kufanya nini na ili uwe nani jibu ambapo atakupatia ni nimekuja chuo kwasababu ya wazazi wangu wametaka nisome au nimekuja kwasababu ya kuwa huru nk.

Ni wanafunzi wachache sana ambao wanatambua kuwa chuo wameenda kufanya nini. Kwanza kabla hujajua nini kimekupeleka chuo ama kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu, kuna maana gani kwako na kwa maisha yako ya badaaye inabidi ujue ufanye nini kabla ya kuingia chuo maandalizi yako kwa ujumla.

Ufanye nini kabla ya kuingia chuo kikuu?

  • Kwanza tafuta kazi ya muda,

Namaanisha kuwa utafte kazi ambayo utaifanya nje ya masomo yako sio lazima kazi hata biashara wewe jiongeze kwa chochote tuu lakini usikose cha kukufanya uwe buzy.

  • Jifunze lugha inayo tumika zaidi chuoni

Baadhi yetu tumetoka santi kayumba so lugha ya kingeleza kwetu ni mtihani soi kabla hujaenda chuo kikuu au chochote jifunze lugha ya kingeleza maana ndo inatumika sana ili usije ukaona chuo kigumu.

  • Chagua course utakayo iweza

Chingine cha kuzingatia ni kuchagua fani ambayo unauhakika nayo ukiipambania itakunufaisha hapo baadae, nimeeleza hii kwasababu kuna baadhi ya marafiki zangu waliacha chuo katikati kwasababu ya kukurupuka, so sitaki nawewe ikukute fanya maamuzi mapema kabla haujachelewa my wangu.

  • Fanya shughuli za kujitolea.

Kufanya shughuli za kujitolea kutakusaidia sana kujulikana na watu mbalimbali, so wewe jitolee tuu kwa chochote usichoke kitakuja kunufaisha baadae I hope.

Kuwa mwanafunzi chuo kikuu kinamaanisha pamoja na kusajiliwa, kuwa na ujuzi, mitazamo, maadili na uwezo hii hukuruhusu kujifunza kwa ufanisi ili kupata matokeo mazuri.

 

Jinsi ya kuwa mwanafunzi mzuri chuoni,

  • Kuwa makini darasani
  • Andika notce kwa kile atakacho kiongea lecture
  • Pitia ulichojifunza kila siku kwa kutumia person time table
  • Fanya kazi uazo achiwa na walimu kwa ufasaha
  • Fuatilia time table ya chuo vizuri, hii itakusaidia kujua siku za test na mitihani ya kumaliza muhura
  • Kutenga muda wa kufurahia maisha, watoto wa mjini tunasema kumwagilia moyo

Kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu kunamaana kuwa, kwanza umeshakuwa mtu mzima na maisha yako yote utayapanga wewe, cha muhimu zaidi ni kujua uko kwa ajili ya maisha yako ya baadae so usichukulie powa kabisa achana na makundi ya watu wasiofaa forcus katika kuitengeneza kesho yako.

Achana na yale maneno kuwa uko chuo kwasababu wazazi wametaka hizi kauli huwapelekea kutokuwa na misimamo katika masomo yenu, I hope mmenielewa kuwa mwanafunzi wa chuo kunamaana kuwa ni mwanzo wa maisha yako na ukipachezea basi kila kitu kitayumba katika maisha yako.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post