Kumbe Tupac hakuwa tajiri

Kumbe Tupac hakuwa tajiri

Tupac Shakur ni moja ya watu maarufu katika historia ya muziki wa hip-hop duniani, hiyo ni kutokana na alama zisizofutia alizoziacha kwenye tasnia ya muziki. Lakini licha ya mafanikio yake, maswali yanabaki juu ya hali yake ya kifedha kabla na baada ya kifo chake.

Wengi hudhani msanii wa hadhi yake angekuwa tajiri mkubwa na wa ajabu, lakini ukweli unaripotiwa kuwa tofauti. Wakati wa kifo chake mnamo 1996, utajiri wake ulikadiriwa kuwa kati ya dola 200,000 sawa na Sh 518,022,602 hadi dola 500,000 sawa na Sh 1,273,764,500.

Kiasi hiki kinatajwa kuwa cha chini sana kwa msanii ambaye aliuza mamilioni ya rekodi na kuigiza katika filamu zilizofanikiwa. Hata hivyo, hali ya kifedha ya Tupac iliathiriwa na mambo mengi, ikiwa ni pamoja na matatizo ya kisheria, matumizi ya kupita kiasi na mkataba usiofaa na lebo iliyokuwa ikimsimamia ya Death Row Records.

Tupac amekuwa mmoja wa watu mashuhuri waliofariki dunia huku wakiwa wamepata pesa nyingi zaidi. Kiwango chake cha utajiri kinaongezeka kutokana na mauzo ya albamu, Digital Platforms, filamu na bidhaa. Kulingana na Forbes, utajiri wa Tupac umeongezeka kwa zaidi ya dola 40 milioni tangu kifo chake na makadirio ya sasa ya utajiri wake ni karibu dola 50 milioni hadi dola 100 milioni.

Inaelezwa iwapo Tupac angeishi na kuendelea na kazi yake, thamani yake ingeweza kufikia mamilioni ya dola. Licha ya umaarufu wake, Tupac alipitia changamoto ya kifedha kabla ya kifo chake. Alikuwa na deni kubwa kwa Rekodi za Death Row, ikijumuisha malipo ya albamu, ada za kisheria na gharama za anasa (pesa za matumizi ya kula bata).

Katika mahojiano ya 1997, mama yake Tupac, Afeni Shakur, alifichua kuwa mwanaye hakuwa na mali nyingi alizojivunia bali zilikuwa chache zikiwemo nyumba na magari yake.

Baada ya kifo chake, mali za Tupac ilibidi kujadiliwa upya kwa haki zake za muziki na vyanzo vya mapato ili kumaliza deni na kuhakikisha kuwa familia yake, pamoja na mama yake, inafaidika na urithi aliouacha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags