Kufanya Ziara Ilikuwa Ni Ndoto Ya Darassa

Kufanya Ziara Ilikuwa Ni Ndoto Ya Darassa

Msanii wa muziki wa Hiphop nchini, Darassa usiku wa kuamkia leo Aprili 26, 2025. amefanya uzinduzi wa ziara ya album yake ya 'Take Away The Pain' Ware House Masaki, jijini Dar Es Salaam.

Katika ziara hiyo ambayo imeanzia Jana usiku iliambatana na pafomance kutoka kwa wasanii tofauti tofauti ambao ni pamoja na Alikiba, Darassa, Bien, Mocco Genius na Marioo.

Akizungumza na waandishi wa habari Darassa muda mchache kabla ya kupanda jukwaani amesema kufanya Shoo hiyo ilikuwa ndoto aliyoota kwa muda mrefu.

"Maisha yetu yote tumekuwa tukiota, Hizi ni ndoto zetu sisi lakini ni ndoto ambazo tunazifanyia kazi sio kwamba ni ndoto ambazo zimelala, kwaiyo kuwepo hapa leo ni moja ya alama ya vitu vikubwa ambavyo.

"Tunavifanyia kazi au ahadi ambazo tunawekeana na Mungu tukiwa tunasali zinakuja kwenye uhalisia na ukweli kwaiyo tumekuwa tukitaka kufanya kwa muda mrefu lakini huu ndio wakati na ndio tumeanza"amesme Darassa.

Darassa amesema kuwa ziara ya album yake haitoishia Dar Es Salaam pekee bali itafanyika na mikoa mingine.

"Baada ya hapa tutakuwa Mwanza Tarehe 3 Mei, 2025, Ntakwenda Arusha mwisho wa mwezi Mei, kwaiyo ntakuwa arround" Amesema Darassa.

Amesema ataendelea kutoa taarifa kuhusu wasanii wengine ambao wataungana nae kwenye ziara yake katika mikoa mingine.

"Tutafanya Love pia kwa watu ambao wananisapoti na tunaendana nao sawa Kwa Dar Bien, Alikiba, Marioo, Jay Melody wote wapo hapa kwa ajili yangu nakubali nguvu yao na niheshima ambayo ntailinda kwa thamani yoyote sana kwa watakao pafomu mbele ntatoa taarifa" Amesema Darassa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags