Konde Ahairisha Show Ya Tukaijaze Nangwanda

Konde Ahairisha Show Ya Tukaijaze Nangwanda

Msanii Harmonize amelazimika kuhairisha show yake iliyopewa jina la ‘Tukaijaze Nangwanda’ iliyotarajiwa kufanyika Januari Mosi 2025 katika viwanja vya Nangwanda mkoani Mtwara baada ya kupata show nyingine nje ya nchi.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa msanii huyo ameleeza miongoni mwa sababu zilizopelekea kuhairisha kwa show hiyo ni ratiba kuingiliana kwani anatakiwa kufanya show nyingine nje ya nchi.

“Tumejitahidi kufanya kila liwezekanalo ndani ya uwezo wetu mpaka kufikia now ila kwamasikitiko makubwa haitowezekana tena tarehe 1/1/2025 kama tulivyo panga poleni sana kwa usumbufufu!!! ratiba za nchi jirani zimeingiliana na Tukaijaze Nangwanda kama mlivyoona tarehe 28 Disemba nilikuwa nchini Uganda tarehe 31 natakiwa niwe Kenya,” ameendika Harmonize.

Mbali na hilo amefunguka kuwa show ya Tukaijaze Nangwanda haikuwa na dhumuni la kutoa burudani pekee bali yeye na timu yake walihitaji kurudisha fadhila kwenye jamii kwa kuwasaidia wazee, vituo vya afya na watu wenye uhitaji.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags