Komasava ya Diamond yafika kwenye chati za Billboard

Komasava ya Diamond yafika kwenye chati za Billboard

Wimbo wa Diamond Platnumz unaotamba hivi sasa uitwao Komasava, umeingia kwenye chati maarufu za muziki nchini Marekani ziitwazo USA Billboard na kuweka rekodi.

Komasava umeingia katika chati hizo ukiwa ingizo jipya na kushika nafasi ya 39 katika Kipengele cha Afrobeats Songs Top 50.

Jambo hilo limeufanya Komasava kuwa wimbo wa kwanza kutoka Tanzania kuingia katika chati hizo kubwa Marekani na duniani kwa ujumla.

Mei 3, 2024, Diamond aliiachia 'audio' ya Komasava ndani yake akiwa amewashirikisha wakali wawili wa Amapiano kutoka Afrika Kusini, Khalil Harisson na Mwanadada Chley.

Baada ya hapo, Diamond akawashtua wengi ilipofika Julai 26 mwaka huu, alipoachia video ya ngoma hiyo ambayo ilikuwa na ingizo jipya ndani yake akionekana muimbaji mashuhuri kutoka Marekani, Jason Derulo aliyeweka vesi moja na kuonekana kwenye video hiyo.

Baada ya hapo wimbo huo uliendelea kukaa katika nafasi za juu kwenye chati mbalimbali za muziki duniani mpaka Agosti 6, 2024 ilipotoboa hadi Billboard.

Wasanii kutoka Nigeria na Afrika Kusini wamekuwa wakitawala kwenye chati hizo ambapo wakati Komasava ikiwa ya 39, mwanadada Tyala kutoka Afrika Kusini ndiye ameshika namba moja na ngoma yake ya Water.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post