Huenda leo isiwe siku nzuri kwa mashabiki wa Liverpool baada ya ‘kocha’ wao Jurgen Klopp kutangaza kung'atuka ‘klabuni’ hapo baada ya msimu huu kumalizika huku akidai ameishiwa nishati za kuendelea kuinoa ‘timu’ hiyo.
Akizungumza jana, #Klopp alisema licha ya mkataba wake wa kuinoa Liverpool kubakiza miaka miwili, ameamua kujiweka kando na kupisha zama mpya, huku akiweka wazi kuwa hana kabisa tatizo lolote na ‘klabu’ hiyo.
Aidha Klopp aliendelea kwa kueleza kuwa anaishukuru ‘klabu’ hiyo kwa sa-poti kubwa ambayo imempa katika kipindi chote alichoinoa hadi kuiwezesha kushinda mataji mbalimbali.
Chini ya Mjerumani huyo, Liverpool imeshinda mataji yote makubwa ambayo baadhi haikuyapata kwa muda mrefu kabla ya ujio wake, yakiwemo Bingwa wa Dunia, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi Kuu ya England na Kombe la FA.
Klopp alijiunga na Liverpool mwaka 2015 akitokea Borussia Dortmund na akiwa na ‘timu’ hiyo ameshinda idadi ya mataji saba.
Hata hivyo, tetesi zinadai kuwa ‘kocha’ huyo huenda akaibukia Bayern Munich ambayo imekuwa ikimtamani kwa muda mrefu ili akachukue mikoba ya Thomas Tuchel.
Leave a Reply