Kipchoge avunja rekodi ya dunia aliyoiweka yeye mwenyewe

Kipchoge avunja rekodi ya dunia aliyoiweka yeye mwenyewe

Mwanariadha bingwa wa mbio za nyika kutoka nchini Kenya Eliud Kipchoge, ameivunja rekodi yake mwenyewe ya dunia katika mbio za nyika za Berlin, Ujerumani.

Kipchoge mwenye umri wa miaka 37, aliweka rekodi mpya ya mbio za nyika kwa muda wa saa 2:01:09, hiyo ikiwa ni sekunde 30 bora zaidi kuliko rekodi aliyoiweka awali ya mwaka 2018 mjini Berlin.

Mkenya Mark Korir alimaliza nafasi ya pili kwa muda wa saa 2:05:58 huku mwanariadha wa Ethiopia Tadu Abate akimaliza wa tatu kwa muda wa saa 2:06:28.

Aidha kwa upande wa wanawake, mwanariadha wa Ethiopia Tigisi Assefa aliibuka mshindi kwa muda wa saa 2:15:37. Mwanariadha mwingine ambaye pia ni Mkenya Rosemary Wanjiru alimaliza wa pili na Tigist Abayechew wa Ethiopia akamaliza wa tatu.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags