Kilichowashinda wasanii wengine, Kendrick kapita nacho kama upepo

Kilichowashinda wasanii wengine, Kendrick kapita nacho kama upepo

Unaambiwa ngoma ya Peekabo inayopatikana kwenye album mpya ya Kendrick Lamar ilimbidi aimbe mwenyewe kiitikio kwani kila msanii aliyekuwa akipewa aimbe alishindwa kutokana na kiitikio hicho kutakiwa kuimbwa haraka kitu ambacho kiliwasumbua wasanii wengi waliojaribu.

Maneno hayo yamethibitishwa na mmoja kati ya rapa aliyehitajika kufanya kiitikio hicho AzChike alipokuwa akifanya mahojiano na Power Fm ambapo alieleza kwa mara ya kwanza aliposikiliza demo ya wimbo huo alihisi ni kitu rahisi angeweza kufanya lakini alipojaribu alishindwa licha ya kurudia mara nyingi. Ndipo alipoamua kubwaga manyanga na kumuachia Kendrick aimbe mwenyewe kiitikio hicho.

"Nilihitajika kufanya kiitikio hicho lakini ilikuwa inahitaji ufundi zaidi kwenye ulimi kutaamka maneno yale. Niliposikia demo yake kwa mara ya kwanza nilishangaa na kujiuliza nani anaimba haraka hivi kwahiyo ilinibidi tu nimwambie Kendrick nimejaribu kutia voko mara nyingi zaidi ila sijaweza kuipata ile standard yenyewe" alisema AzChike

Peekaboo ni Track namba 9 kwenye album mpya ya Kendrick iliyotoka kwa kushtukiza Novemba 22, 2024 ikiwa na jumla ya ngoma 12 ambapo mpaka sasa inaendelea kukimbiza kwenye majukwaa mbalimbali ya kuuzia na kusikilizia muziki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags