Kesi nyingi za ukatili dhidi ya wanawake haziripotiwi

Kesi nyingi za ukatili dhidi ya wanawake haziripotiwi

Hayo yamebainishwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ambapo ameviagiza Vyombo vya Dola viongeze nguvu kupambana na kudhibiti Ukatili dhidi ya Wanawake, Watoto wa Kike na wa Kiume

Mpango amesema matukio ya Ukatili dhidi ya Wanawake yaliyoripotiwa kwa mwaka 2021 yalikuwa 20,897 na mwaka 2020 yalikuwa 28,126 na kwamba zipo kesi nyingi ambazo hazikufika kwenye Vyombo vya Dola

Aidha, Takwimu za Jeshi la Polisi za mwaka 2021, zinaonesha kulikuwa na matukio 5,899 ya Ubakaji, Mimba za Utotoni 1,677 na matukio ya Ulawiti 1,114.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post