Kenya yaiweka Tanzania katika orodha ya wazalishaji 10 bora wa parachichi

Kenya yaiweka Tanzania katika orodha ya wazalishaji 10 bora wa parachichi

Parachichi katika siku za hivi karibuni limekuwa moja ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi huku wakulima wengi wakishiriki katika kile ambacho kimebatizwa kama dhahabu ya kijani.

Licha ya kwamba uzalishaji umefikia kiwango cha juu zaidi, Tanzania bado haijaingia katika orodha ya wazalishaji 10 wa kimataifa huku uzalishaji mkubwa ukitawaliwa na nchi za Kusini na Amerika ya Kati.

Kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya ulimwengu wa takwimu, Kenya ndiyo nchi pekee barani Afrika katika wazalishaji 10 bora wa Parachichi yenye tani 176,045 kila mwaka.

Huku nchi inayoongoza kwa uzalishaji ikiwa ni Mexico yenye tani 1,889,354, Jamhuri ya Dominika yenye tani 601,349, Peru 455,394, Colombia tani 309,431 na Indonesia tani 304,938 kwa mwaka.

Tanzania Horticultural Association (TAHA) inakadiria kuwa mauzo ya parachichi nchini yalifikia tani 11,237, au makontena 510 yenye thamani ya dola milioni 33 mwaka 2021.

Hii ni asilimia 12.6 zaidi ikilinganishwa na mauzo ya 2020. Kwa mujibu wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), mwaka 2018 Tanzania ilisafirisha tani 7,551 zenye thamani ya jumla ya dola milioni 8.5 kwenda Ulaya, Afrika na Asia.

Uzalishaji huo wa kibiashara/usafirishaji wa parachichi nje ya nchi unatawaliwa na Kampuni ya Rungwe Avocado Ltd na Africado Ltd, ambapo maskani yake ni Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro na kampuni hizo mbili kwa pamoja huzalisha zaidi ya tani 5,000 kwa mwaka.

Ikumbukwe tu maeneo maarufu Tanzania yanayozalisha parachichi yapo katika mikoa ya Mbeya, Njombe, Songwe, na Iringa upande wa kusini-magharibi, na Kilimanjaro, Arusha, na Tanga kaskazini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags