Kanuni za kufuata ili mazoezi yako yawe bora

Kanuni za kufuata ili mazoezi yako yawe bora

Leo katika fitness tumekuwekea kanuni 10 za kufuata ili mazoezi yako unayoyafanya yawe bora na kuleta faida na manufaa katika mwili.

Kanuni hizo ni hizi zifuatazo:

  1. Mazoezi yako yanatakiwa yaendane na wewe usifanye mazoezi kwa kumuiga mtu mwingine. Angalia uwezo wako wa kufanya mazoezi na endana na uwezo wako. Usitake kukimbia kama mwanariadha wakati hata kutembea tu kwako ni shida.
  2. Fahamu lego la mazoezi yako ni nini?, unahitaji nini kwenye mazoezi?, na uwezo wako ni upi?.
  1. Mazoezi ili yaingie kwenye mwili inatakiwa uzidishe kidogo, iwe tofauti na kawaida yako. Uzidishe kwa kufanya mara kwa mara, kufanya kwa kwa nguvu zaidi, kubadili aina ya mazoezi au kwa kuongeza muda wa kufanya hilo zoezi. Kifupi, unapohisi kuchoka ongeza kidogo.
  1. Endelea kuongeza kiwango cha kufanya mazoezi, taratibu taratibu kila siku. Yaani kama ulikuwa una piga pushapu kumi, kesho fanya kumi na moja n.k.
  1. Fanya mazoezi tofauti tofauti, usifanye zoezi la aina moja tu, hii husaidia kwamba usiboreke na mazoezi.
  1. Pata muda wa kupumzika, nashauri, walau siku mbili za wiki. Hii pia huusaidia mwili kuendana vizuri na mazoezi unayofanya.
  1. Usiache mazoezi. Unapoacha mazoezi, uwezo wako wa kufanya mazoezi hupungua na hatimaye hupotea kabisa.
  1. Ukishakuwa vizuri (Fit), unaweza endelea kufanya mazoezi kwa kiwango hicho hicho ulichofikia au hata ukipunguza kidogo inakuwa haina shida sana kwa sababu mwili unakuwa ushapokea mazoezi vizuri.
  1. Unapokuwa vizuri sana kwenye mazoezi, uwezo wa mwili kupokea mazoezi unapungua kidogo kwa sababu mwili unakuwa tayari ushakua fiti, ingawa haushauriwi kuacha mazoezi kwa sababu ukiacha uwezo wako unapungua.

Hizo ndo kanuni nami kuanzia leo naanza rasmi kuzifuata.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags