Kanisa nchini Ethiopia lamkosoa Waziri Mkuu wao

Kanisa nchini Ethiopia lamkosoa Waziri Mkuu wao

Uongozi mkuu wa Kanisa la Kiorthodox nchini Ethiopia (Synodi), ambalo ni Kanisa kubwa zaidi nchini humo, umetishia kuitisha mikutano ya kitaifa itakayoongozwa na mkuu wa Kanisa Hilo, Abuna Mathias.

Kanisa hilo limekosoa kauli za hivi karibuni za Waziri Mkuu Abiy Ahmed kuhusu makasisi wakorofi waliohusika katika uteuzi wa maaskofu bila uelewa.

Hotuba ndefu ya Abiy, iliyotangazwa kwenye televisheni ya taifa, ilitolewa baada ya sinodi ya kanisa hilo kuwatenga makasisi, ambao wanatoka katika jimbo la Oromia nchini humo.

Aliwaonya mawaziri wake dhidi ya kujihusisha na masuala ya kanisa. Hata hivyo, alisema kila upande ‘’una ukweli.”

Sinaodi ilieleza kuwa kauli za Waziri mkuu zilipuuza maamuzi yake na kukosoa mamlaka yake na kulitambua kundi “lisilo halali lenye njaa ya madaraka."

Kundi la maaskofu waliojitenga linalishutumu kanisa kwa kushikilia mfumo wa lugha na utamaduni na mamlaka ambapo kanisa la Oromia waumini hawafundishi kwa lugha zao za asili. Kanisa limekanusha shutuma hizo.

Makasisi waliojitenga walisema “walizidiwa ” na uungaji mkono wa umma baada ya kutembelea baadhi ya maeneo katika jimbo llililokumbwa na mzozo la magharibi mwa Oromia.

Taarifa ya sinodi inakuja huku kukiwa na shutuma miongoni mwa waumini kwamba mamlaka zinawaunga mkono makasisi waliojitenga.

Uhusiano baina ya utawala wa Bw Abiy na kanisa lenye waumini karibu nusu ya milioni 110 ya raia wa Ethiopia umekuwa ukizorota licha ya kwamba ulikuwa mzuri katika siku za mwanzo za uongozi wake.

Aidha uhusiano wa pande mbili ulizorota zaidi wakati wa vita vya Tigray baada ya Askofu Abuna Mathias kuzungumza dhidi ya kile alichokiita mauaji ya kimbari.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags