Kampuni zinazofanya kazi na Diddy kuchunguzwa

Kampuni zinazofanya kazi na Diddy kuchunguzwa

Wakati baadhi ya ma-staa mbalimbali wakihusishwa katika kesi ya mwanamuziki Diddy, na sasa imeripotiwa kuwa Mamlaka inayojihusisha na uchunguzi wa kesi hiyo inatarajia kufanya uchunguzi kwa watu wote wa karibu wa Combs.

Kwa mujibu wa Tmz imeeleza kuwa makampuni pamoja na Taasisi ambazo zilikuwa zikifanyabiashara na Diddy wanatarajiwa kutumiwa wito wa kufika Mahakamani wiki hii kwa ajili ya uchunguzi.

Wito huo pia utatolewa kwa mashirika ya ndege ya kibiashara, ambayo Diddy aliwahi kutumia ndege zao katika safari zake badala ya kutumia ndege yake binafsi.

Mpaka kufikia sasa imeelezwa kuwa tayari watu kadhaa ambao wamehusishwa katika kesi ya Diddy wameshafanyiwa mahijiaono, huku mamlaka hiyo ikieleza kuwa huenda kesi ikachukuwa muda kutokana na kutokuwa na ushahidi wa kutosha.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post