Ooooooh! Kama tunavyojua msimu wa siku kuu za Krismasi huwaleta ndugu jamaa na marafiki pamoja katika mikusanyiko kama hiyo vyakula na vinywaji vya kila aina huandaliwa ili kunogesha siku hizo.
Nyakati kama hizi baadhi ya watu wanakabiliwa na kibarua kigumu kufuata utaratibu wao wa kawaida hasa katika masuala ya lishe. Kutokana na hilo mtindo wa maisha hubadilika na hapo ndipo uzito wa mwili pia uweza kubadilika.
Ni nyakati hizi pia ambapo utasikia kusikia jamaa na marafiki wakiwa na wana mazoea ya kusema "nitaanza kesho", msemo ambao unaweza kuendeleza tabia zisizofaa.
Lakini je unawezaje kufurahia msimu wa Krismasi bila kuathiri mpango wako wa afya?
Kwanza kabisa ukiwa na nia ya dhati ya kudhibiti uzani wako lazima ujiwekee mipaka katika ulaji wako ili kuimarisha malengo yako, anasema mtaalamuwa lishe bora Irine Nduta kutika Kenya.
''Ni vyema kuachana na mienendo ambayo haiendani haziendani na malengo yako.''
Ili usiongeze uzani kupita kiasi msimu wa siku kuu za Krismasi na mwaka mpya zingatia vidokezi hivi vitano.
- Chagua vyakula usile kila kitu
Ni muhimu pia kufahamu kuwa unaweza kuteleza mara moja au mbili katika safari hii ya kudhibiti uzani anasema mtaalamu wa lishe bora Bi Nduta. Mara nyingi watu huachana na malengo yao baada ya hili kutokea.
Lakini, ni bora kuendelea kuzingatia lishe bora kuliko kurudi nyuma.
- Kula kwa kipimo
Punguza vyenye wanga katika sahani yako ikiwezekana kwa karibu theluthi tatu, kile kinachoitwa sheria ya udhibiti wa chakula ili kuboresha afya.
Unaweza kifikia lengo hili kwa kujizoesha kula chakula kidogo kwa saa chache za siku au kufunga na kula katika masaa manane kwa siku au kufunga kula chakula siku mbili kwa wiki.
Hii ni mambo yanayoaminiwa kupunguza hatari ya kupata magonjwa yanayohusiano na umri.
- Jifuatilie mwenyewe
Ingawa kuzingatia malengo ya kudhibiti uzani kunaweza kuwa kibarua kigumu wataalamu wa masuala ya afya wanasema.
Ni vyema kuhakikisha kuwa unapunguza ulaji wa vyakula vya vilivyokaangwa kwa kutumia mafuta mengi wakati wa likizo.
- Fanya mazoezi
Maisha ya kutofanya mazoezi ya mwili husababisha 10% ya vifo vya mapema vinavyotokana na magonjwa kama vile ugonjwa wa moyo, kisukari aina ya mbili, na aina mbali mbali za saratani.
Hakikisha unatembea au kuogelea hali ya hewa ikiauhusu, na epuka kutumia kipindi cha sherhe kukaa mahali pamoja.
- Usinywe pombe
Epuka vinywaji baridi na pombe kupita kiasi kila siku.
Unapokunywa pombe hakikisha unakunywa maji pia kati ya kila kinywaji cha pombe.
Haya haya wale wenzangu na mie wanaopenda kula harafu hawapendi mkunenepa wakatiwenu ni huu sasa, so zingatia kila utakacho kula ili mwili mwako uweze kuwa sawa kama utakavyo.
Leave a Reply