Kajala ataja sababu za kuwepo kwenye video ya Harmonize

Kajala ataja sababu za kuwepo kwenye video ya Harmonize

Ebwana mambo vipi? Kitu juu ya kituu hatarii aiseee. Baada ya Mmakonde kuachia ngoma mbili kwa wakati mmoja, basi bhana moja ya stori iliyozua mjadala kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusu video ya wimbo wa ‘Nitaubeba’ ambapo katika video hiyo mwanadada Kajala alionekana.

Nikukumbushe tu kuwa Kajala ndio meneja wa Konde Boy na kupitia ukurasa wake wa Instagram ametaja sababu za yeye kuwepo kwenye video hiyo na kusema huo wimbo ameimbiwa yeye.

“I had to do this video because my hommie sang it for me. I love you so much hommie, you're the best thing I ever had,” ameandika Kajala.

Aidha haikuishia hapo, baada ya kuandika ujumbe huo Mmakonde hakuwa mbali, akashusha comment yenye ujumbe wa mahaba kwenye ukurasa wa meneja wake ukiwa unasema,

“Umekuwa na mchango mkubwa sana kwenye maisha yangu tangu uliponiambia umenisamehe and you're ready to take me back. Nimekuwa mtu mpya yes, I feel brand new, naiona nguvu ya mapenzi yako kwangu almost 6 months, haijapita masaa 5 kabla hatujaonana au hatujaongea kwa simu.”

Pia Harmonize akaongezea kuandika, “Nikisema hatugombani nitakuwa muongo maana mapenzi bila kununiana, kudekeana hayanogi especially you, tunaongea almost kila kitu utani, ujinga, umbea na ushenzi, just know that you mean eveyrthing to me and i did this for you, for someone I love na kwa wote wanaopendana thanks for everthing you done to me. I love you.”

Vilevile akamalizia kuandika, “this one is another memory kuwaonyesha mapacha baadae how we love each other.”

 

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post