Justin Bieber auza haki za nyimbo zake

Justin Bieber auza haki za nyimbo zake

Muwimbaji nguli na mtunzi wa nyimbo Justin Bieber ameuza sehemu ya haki ya muziki wake kwa kampuni ya muziki ya Hipgnosis Songs Capital kwa dola milioni 200.

Kampuni hiyo sasa inamiliki hisa za mwimbaji huyo wa pop katika baadhi ya nyimbo maarufu zaidi za miaka ya hivi karibuni  ikiwa ni pamoja na "Baby" na "Sorry."

Bieber ni miongoni mwa wa wasanii wenye mauzo makubwa ya nyimbo zao katika Karne ya 21, anajiunga na kundi la wasanii ambao wamepata pesa kupitia albamu zao.

Hatua hiyo inamaanisha kuwa kampuni ya Hipgnosis itapokea malipo kila wakati wimbo wanaomiliki sehemu yake unapochezwa kwa umma. Kampuni hiyo ilipata haki miliki za uchapishaji wa nyimbo za Bieber kwenye albamu yake yenye nyimbo 290.

Hiyo inajumuisha muziki wake wote uliotolewa kabla ya tarehe 31 Desemba 2021 na sehemu ya mwandishi wake. Haki za msanii nyota huyo kwa rekodi zake kuu (master recordings) pia zimewekwa katika mpango huo.

Hipgnosis haijaweka wazi masharti ya mkataba huo, lakini chanzo kililiambia shirika la habari la AFP kuwa ilikuwa na thamani ya karibu dola milioni 200.

Wasanii wanazidi kuuza hisa za kazi zao kwa kampuni za muziki  ikiwa ni pamoja na Justin Timberlake na Shakira, ambao pia wameingia mkataba na Hipgnosis.

Lakini hali hiyo ni ya kawaida zaidi kwa wasanii wakubwa. Katika miaka miwili iliyopita, nguli wa muziki Bob Dylan na Bruce Springsteen wote waliuza haki za albamu zao kwa kampuni ya Sony.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post