Jordan na Amber sio wapenzi

Jordan na Amber sio wapenzi

Tetesi zilizoibuka siku za hivi karibuni zikidai kwamba muigizaji Michael B. Jordan kudaiwa kutoka kimapenzi na mwanamitindo wa Uingereza Amber Jepson sio za kweli.

Kwa mujibu wa TSR, chanzo cha karibu kabisa cha muigizaji huyo kilisema uwa wawili hao wala hawana hawako katika mahusiano na sio wapenzi kabisa kwani hawajawahi hata kukutana kabla.

“He is not secretly dating 26-Year Old British Bikini Model Amber Jepson. A close reliable source To The Creed III told The shade room that This Rumor Is "Untrue" as "The Two Have Never Met Before.”

Ikumbukwe tu kuwa Jarida la The Sun ndio kilikuwa chombo cha kwanza kuripoti taarifa hii wakisema kwamba wawili hawa walikuwa katika hatua za awali za uhusiano wao na wamekuwa kwenye miadi nyingi wakati Michael B. Jordan akiwa nchini Uingereza, kufuatia ununuzi wake wa hisa kwenye klabu ya soka AFC Bournemouth hivi karibuni.

Hivyo basi The Shade Room imethibitisha na kukanusha taarifa hii ambayo imekuja miezi 6 tu tangu Micahel B. Jordan aachane na mpenzi wake Lori Harvey.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post