Joel Lwaga aendelea kuwakalisha wasanii wa Bongo Fleva

Joel Lwaga aendelea kuwakalisha wasanii wa Bongo Fleva

Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Joel Lwaga ameendelea kuonesha ubabe wake kwenye mtandao wa kusikiliza muziki wa Apple Music kwa kuendelea kushika namba moja kwa wiki tatu mfululizo.

Lwaga ameendelea kuwa na ushawishi mkubwa katika mtandao huo kupitia wimbo wake wa ‘Olodumare’ huku akiwakalisha wasanii wakubwa katika chati hiyo akiwemo, Marioo, Diamond, Jux, Zuchu na wengineo.

Wimbo wa ‘Olodumare’ ambao kwa sasa unazidi kupenya katika mataifa mbalimbali, kupitia mtandao wa YouTube umetazamwa zaidi ya mara milioni 1.7 ukiwa na mwezi mmoja tu tangu kuachiwa kwake.

Kupitia wimbo huo kuwa mkubwa baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva na Hip-hop nchini wameingizia mistari yao akiwemo Bando, Anko Mwange na Malume.

Mbali na ngoma hiyo mpya Joel amekuwa akifanya vizuri na nyimbo zake nyingine kama Sitabaki kama Nilivyo, Yote Mema, Umenishangaza, Umejua Kunifurahisha, Mimi ni wa Juu na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags