Jela miaka 18 kwa kosa la kujiteka

Jela miaka 18 kwa kosa la kujiteka

Oooooohooooo! Naona maisha yanazidi kuwa magumu mpaka tunaamua kujiteka wenyewe duuuh! Basi bwana kuna mwanamke mmoja amezua taharuki kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari baada ya kuhukumiwa jela kwa kosa la kujiteka mwenyewe.

Mwanamama huyo kutoka California ambaye alifeki utekaji nyara wake binafsi amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela kwa kutoa taarifa za uongo kwa FBI. Sherri Papini mwenye umri wa miaka 39, alipotea Novemba 2016 baada ya kwenda kukimbia.

Alionekana wiki tatu baadaye na siku ya kutoa shukrani alizungumza na kudai kuwa wanawake wawili wa Kihispania walikuwa wamemteka nyara na hivyo kuzua msako wa mataifa mengi.

FBI baadaye ilihitimisha kuwa alikuwa akiishi katika nyumba ya mpenzi wake wa zamani na alikuwa amejijeruhi kama sehemu ya mpango huo.

“Ninasikitika sana kwa watu wengi ambao wameteseka kwa sababu yangu - watu waliojitolea kwa hiari kunisaidia katika wakati ambao nilihitaji sana msaada,’’ alisema Ms Sherri.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post