Jela maisha kwa kubaka mtoto wa mkewe

Jela maisha kwa kubaka mtoto wa mkewe

Mahakama ya Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha imemuhukumu kifungo cha maisha, John Sanare Lukuaya Mkazi wa Kijiji cha Kimnyaki, kwa kosa la kumbaka Mtoto wa miaka mitatu na miezi miwili ambaye inadaiwa ni Mtoto wa Mke wake.

Akitoa hukumu hiyo jana January 04, 2023 Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya, Gwantwa Mwankunga, amesema Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yoyote na kumtia hatiani kwa kosa la kubaka.

Mwendesha mashitaka na Wakili wa Serikali Penina Ngotea, aliieleza Mahakama hiyo kuwa Mtuhumiwa alitenda kosa hilo tarehe 10 Julai ,2022 katika Kijiji cha Kimnyaki ndani ya nyumba wanayoishi na Mtoto huyo, ambapo alimbaka na kumsababishia maumivu makali.

Mwendesha mashtaka huyo, amesema Mtuhumiwa alimbaka mtoto huyo muda wa usiku wakati Mama wa Mtoto huyo akiwa amekwenda kulala kwenye msiba wa Jirani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags