Jeans kongwe duniani yauzwa kwa dolla

Jeans kongwe duniani yauzwa kwa dolla

Suruali ya kiume ambayo maafisa wa mnada wanaamini kuwa inaweza kuwa ndio jeans kongwe zaidi duniani imeuzwa kwa dola 114,000 (£92,010).

Suruali hiyo ilipatikana baharini kwenye meli iliyozama baada ya kupata ajali mwaka 1857 huko karibu na pwani ya North Carolina.

Suruali hiyo ina vifungo vitano na inaaminika kuwa ni mali ya mchimba migodi.

Mnada huo ulifanyika Reno, Nevada magharibi mwa Marekani, na pia mtandaoni, tarehe 3 Desemba.

Meli hiyo ilizama wakati wa vimbunga viwili mnamo Septemba 1857, na kuua abiria 425 kati ya 578 na wafanyikazi.

Abiria walizama wakiwa na takriban tani 21 za sarafu za dhahabu na vitu vya kale. Ajali hiyo iligunduliwa kwa mara ya kwanza mnamo 1988.

Suruali hiyo lipatikana kutoka katika sanduku la John Dement, mwanamume kutoka Oregon, ambaye huenda aliinunua huko San Francisco, kampuni ya mnada ilisema.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags