Japan kuzindua roboti anayecheka kama binadamu

Japan kuzindua roboti anayecheka kama binadamu

Wanasayansi kutoka Japan wako mbioni kuzindua roboti lenye ngozi hai ambalo litakuwa na uwezo wa kucheka pamoja na kutabasamu kama binadamu.

Ubunifu huo ulioongozwa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Tokyo, wameweka wazi kuwa walilifanikisha hilo kwa kupandikiza tishu zipatikanazo kwenye ngozi ya binadamu.

Hata hivyo watafiti hao wamedai kuwa ngozi hiyo inautofauti kidogo kwani licha ya kuwa laini lakini inauwezo wa kujiponya yenyewe pale ipatapo majeraha.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali vinaeleza kuwa Japan ndio nchi ya kwanza kuzindua roboti mwenye ngozi hai huku watafiti hao wakiitoa kimasomaso nchi hiyo katika ukuaji wa Teknolojia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post