Ijue kazi yenye manufaa baadae

Ijue kazi yenye manufaa baadae

Mambo vipi kijana wenzangu, leo Jumatatu tulivu kabisa katika karia tunakuletea mchongo mmoja matata sana ambao ukiufahamu basi ukimaliza tu masomo yako na ukaufanya  lazima utoboe.

Mchingo huo si mwingine ni kazi zenye manufaa makubwa huko baadae ambapo sisi tumeona ni kazi ya ujasilimali wa vitu mbalimbali kadiri ambavyo wewe unapenda.

Naomba kwanza uelewe kuwa kwa mujibu wa ripoti ya ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kiuchumi na kijamii (DESA) iliyotolewa Julai mwaka jana ilitaka nchi ziondoe vikwazo ambavyo vinawazuia vijana kuwa wajasiliamari wenye mafanikio.

Ripoti hiyo ya dunia ya vijana kwa mwaka 2020 iliyopewa jina “Ujasiriamali wa kijamii kwa vijana na ajenda 2030” ilitoa wito kwa serikali na wadau wengine wafanyamaamuzi “kuondoa vikwazo kwa ujasiriamali kwa vijana kama vile fursa ya kupata mitaji ya kuanzia ambayo kwa sasa ni adimu na inawazuia vijana wengine kujihusisha katika shughuli mbalimbali zinazoweza kuwaletea faida.”

Ripoti hiyo iliongeza kuwa mifumo mingi ya ufuatiliaji pia mara nyingi inakuwa kikwazo ama bila kujua inawakosesha vijana wengi kupata fursa za mikopo ya kifedha na huduma zinazohitajika kuanzisha shughuli za ujasiriliamali.

 

Na uhaba wa fursa za mafunzo, msaada wa kiufundi, mitandao na masoko vilielezwa na ripoti hiyo kuwa ni sababu zingine zinazowakatisha tamaa vijana kuanzisha miradi.

Pamoja na hayo yote niliyokueleza mimi dhumuni langu ni kukueleza kuwa ujasilimali ndio mchongo utakaokufanya uwe na mafaniko huko mbeleni.

Kama kweli kijana wenzangu ukiamua na kujikita katika kufanya ujasriamali mbambali jambo hilo litakufanya upate fedha  za kujikimu pindi unapokwa chuoni.

Huko chuoni ulipo sasa hakikisha unafikiri aina ya biashara ndogo ndogo unayoweza kuifanya ili uweze  kujiingizia kipato hicho  ambacho kitaweza kuwapunguzia majukumu wazazi ya kukuhudumia.

Ni ukweli uliyowazi kuwa ujasiriamali ndio kazi pekee inayoweza kudumu kwa muda mrefu kama ukiipangilia vizuri na kuifanya kwa malengo. 

Badilika sasa kijana changamkia kila fursa za ujasiriamali zinazokuja mbele yako, acha kukaa kizembe tambua kuwa utegemezi wala sio dili  kwa sasa, fanya maamuzi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags