Ifahamu jamii inayokunywa supu iliyochanganywa na majivu ya marehemu

Ifahamu jamii inayokunywa supu iliyochanganywa na majivu ya marehemu

Tamaduni ni nyingi ulimwenguni na nyigine ni za ajabu, lakini pamoja na uajabu wake hugeuka na kuwa kuvutio kwa baadhi ya watu na ndiyo maana imekuwa kawaida kukuta jamii fulani ikienda kutalii kwenye jamii nyingine.

 

Kila jamiii, huwa na tamaduni zake katika upande wa mazishi, kuna zile tamaduni ambazo watu huzisikia tu na kuziona kwenye sinema, leo acha tuelezane machache kuhusiana na tamaduni ya jamii ya Yanomami.

 

Jamii hii hufanya tamaduni ya kuchoma mwili wa marehemu na kisha majivu ya mwili huo huchanganywa kwenye supu na kisha hunyewa na watu msibani.

 

Jamii hii inapatikana Brazil na Venezuela, ambayo watu wake wamejikita kuishi msituni na imekuwa ngumu sana kwao kubadili utamaduni wao, katika mazishi ya mpendwa wao basi huchoma mwili wake na kukusanya mifupa ambayo huisaga na unga wake kuweka pamoja na majivu ambayo huchanganywa kwenye supu.

 

 

Supu hiyo kawaida yake huwekewa na vipande vya ndizi  na mchanganyo huo wa majivu. Hata hivyo jamii hii hufanya hivyo msibani kwa imani ya kuwa wanalinda mwili wa ndugu yao baada ya kufariki.

 

Na endapo mtu akifariki kwa kuuawa basi wanawake pekee ndiyo hutakiwa kunywa supu iliyochanganywa na majivu ya marehemu huyo, na kisha siku hiyohiyo watu wa tamaduni hiyo huenda kulipiza kisasi kwa watu waliofanya mauaji.

 

 

 

 

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags