Hivi ndivyo mitandao ya kijamii inavyowapa fursa watu

Hivi ndivyo mitandao ya kijamii inavyowapa fursa watu

Mitandao mitandao mitandao, nimeiiita mara tatu, watu wengi siku hizi wanatumia mitandao kama sehemu ya ku-post maudhui yasiyofaa na kufanya kuwa kilinge cha umbea na kufuatilia maisha ya watu.

Lakini kuna baadhi yao wamejitambua na kujua kuwa mitandao ya kijamii ni fursa katika kuwaingizia vipato na kuwatengenezea jina ambalo linawasaidia katika shughuli na biashara zao.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara zinazofanya vizuri katika matumizi ya mitandao ya kijamii. Na hii inachagizwa na ongezeko la watumiaji wa simu janja na huduma ya mtandao (intaneti) nchini.

Mitandao hii si tu majukwaa ya kimawasiliano, bali ni fursa katika ulimwengu wa leo ya kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla endapo itatumika vizuri.

Licha ya kuwa na idadi kubwa ya watumiaji wa huduma za intaneti na simu janja, lakini matumizi ya mitandao ya kijamii yameendelea kuwa kitendawili kwa Watanzania wengi.

Wapo ambao wamekuwa wakiitumia mitandao hiyo kwa namna sahihi ambayo imekuwa ikiwanufaisha kama vile kibiashara, kikazi na kielimu na wale ambao wamekuwa wakiitumia ndivyo sivyo.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumeshuhudiwa kukithiri kwa matukio ya upotoshwaji wa taarifa, wizi mitandaoni, usambazaji wa maudhui yasiyo na maadili (picha na video za utupu na lugha za matusi) na udhalilishaji yanayofanywa mitandaoni.

Kwetu Mwananchi Scoop kama kawaida yetu hatunaga jambo dogo tukakutana na mfanyabiashara ambaye biashara zake huwa anazifanya mitandaoni, ambapo bidhaa na biashara zake zote anazitunza nyumbani kwake kutokana na kuwa na mtaji mdogo wa kumfanya kushindwa kulipia fremu.

Amina Salum ambaye ni mkazi wa Gongo la Mboto yeye ameeleza kuwa ametumia mitandao yake ya kijamii ya Instagram na Tiktok kutangaza biashara yake na madera kutoka Mombasa na huwa anafanya biashara hiyo kwa kufanya delivery kwa yule anayehitaji bidhaa hizo.

Aidha aliendelea kwa kueleza kuwa licha ya kukumbana na changamoto kufuatiwa na biashara hiyo lakini hajawahi kukata tamaa ambapo ameeleza kuwa baadhi ya wateja anaweza akakupigia simu na kukwambia umpelekee mzigo sehemu fulani ukaharibu nauli kufika sehemu husika usimkute mtu na simu hapokei.



Kwa upande wake ameeleza kuwa mitandao imemnufaisha kwa kuwa biashara inaenda faida anapata na wateja pia kutoka katika mikoa mbalimbali.

Hivyo basi amewataka vijana na wamama wa nyumbani kuacha kupoteza muda kufuatilia masuala ya udaku katika mitandao na waamke sasa na watumie mitandao hiyo vizuri.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post