Hivi hapa Vyakula vya kuongeza Nguvu za Kiume

Hivi hapa Vyakula vya kuongeza Nguvu za Kiume

Weeeuuuweeee! Kama mnavyo jua jana kulipigwa marufuku ya matumizi ya unga wa kuongeza nguvu zakiume inayo julikana kama Vumbi la Kongo, basi bwana leo tumekuletea jambo nyetii yaaani hutoboreka kulisoma, tunakuletea vyakula mbali mbali ambavyo vitaweza kukusaidia wewe kijana ulie athirika na dawa ya mkongo.

Usipoteze tena gharama kubwa ya kununua vitu ambavyo vitakuletea madhara badae bali anza kwa kutumia vitu asili ambavyo vitakupa ngvu hizo unazo zitafuta kwa miaka yote ya maisha yako, tunakusogezea vyakula ambavyo ni rahisi kuvipata kwa ajili ya afya yako.

Vyakula na Njia za kuongeza nguvu za kiume haraka

  1. Ndizi

Wakati unafikiria uwezo wa kufanya vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye muhimu katika kujamiiana. Kwa msingi huo ulaji wa ndizi mbivu ndani mwake kuna Vitamin B inatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa hodari na nguvu Zaidi za kufanya tendo bila kuchoka.

  1. Mbegu za maboga

Kitu chingine ambacho kinaongeza nguvu za kiume ni unga na mbegu za maboga ambazo ni rahisi kabisa kuzipata zinauzwa kila kona, Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.

Mbegu hizi ambazo zinamadini ya chuma zinashusha kisukari, zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya zaidi ni kuwa zina madini ya Zinki madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili. Unatumia katika kutafuna mahali popote sio chungu ziko kama karanga tuu kwa wale wasizo zifahamu au unga wake unaweka kwenye uji ama chai. 

  1. Pilipili

Pia pilipili unaweza changanya kwenye chakula au ukala hivyo hivyo kwani zinasaidia mzunguko mkubwa wa damu kwa maana hiyo kufanya kuwa na hisia kali za mapenzi kwa hiyo pili pili ni chachu ya kuuamsha hisia, pia kwa mwanamke inamsaidia kuongeza joto ukeni, haishauliwi kutumia nyingi Zaidi.

  1. Tangawizi

Tangawizi ni moja ya Chakula kinachoweza kurejesha Nguvu za Kiume, unaweza kuichemsha Tangawizi na ukatumia kwa kuinywa kama chai asubuhi, mchana na jioni pia unaweza ukaitumia katika mchanganyiko wa kiasili kwa kutumia Habat Soda, Asali, Kitunguu Swaumu na Tangawizi Yenyewe.

Tangawizi husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini,  kwa hivyo, ni bayana kuwa kiungo cha mwanamume kinachoshiriki tendo la ndoa kitakuwa na damu ya kutosha na pia kusimama kwa muda mrefu. Pia, ulaji wa tangawizi husaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa.

  1. Shiriki tendo la ndoa mara nyingi

Kuna stori zinasema twiga hakuzaliwa na shingo ndefu namna hii kama anavyoonekana akiwa mkubwa, bali wanasema ile tabia yake ya kupenda kula majani ya juu ya miti ndiyo ikapelekea shingo yake ikarefuka!. Inawezekana kuna ukweli kidogo wa stori hizi. Usinielewe vibaya wala usije ukasema huyu jamaa anahamasisha watu kufanya mapenzi! Hapana usiwe na haraka hivyo utanielewa tu ninachotaka kusema

Wanasayansi wa masuala ya mapenzi wanasema ikiwa mtu mzima hana msongo wowote wa mawazo (stress), ana afya nzuri tu ya kutosha na anakula vizuri basi anaweza kushiriki tendo la tendo kila baada ya masaa 24.

  1. Asali yenye mdalasini

Vinapoungana vitu hivi viwili hufanya dawa moja mhimu sana ya kuongeza kinga ya mwili. Kunywa chai yenye asali na mdalasini mara kwa mara kunaongeza kinga ya mwili, nguvu ya mwili na nguvu ya ubongo kwa pamoja.

Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 8 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja. Acha ndani ya bakuli kubwa ili iwe rahisi kuikoroga vizuri kila unapoitumia. Lamba vijiko vikubwa vitatu kila unapoenda kulala. Fanya hivi kwa mwezi mmoja.

  1. Pweza na chaza

Aina hizi za samaki zinazovuliwa baharini huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalisha wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa.

Wataalam na wanasayanzi wa ndani kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili na wa Kimataifa wamethibitisha kuwa supu ya pweza ina uwezo wa kuongeza nguvu za kiume.

Wataalam hao wanadai kuwa supu hiyo inafanya kazi hiyo kwa asilimia kubwa tofauti na madawa kama mkongo na mengineyo.

  1. Kahawa

Kutumia kahawa kupita kiasi kunaweza kusiwe kuzuri kwa afya yako.Lakini hatukatai kwamba kafeini iliyomo kwenye kahawa inaweza kukupa nguvu nyingi sana za kuweza kuchelewa kufika kileleni mapema, Tumia kwa busara kwani kinaweza kikawa kina faida na hasara kwa upande mwingine pia.

  1. Chocolate


Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwasababu ina viambato vya phenylethylamine na alkaloid. Phenylethylamine ni kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa wakati wa kufanya mapenzi na alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati wa mapenzi.

  1. Siagi ya Karanga na karanga zenyewe

Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.

Siagi ya karanga ina kiasi kingi cha mafuta masafi yasiyoweza kusababisha kolesto/lehemu mwilini (unsaturated fats) na kiasi kingi cha protini, vitu hivi viwili vinafanya kazi ya kuongeza nguvu mwilini. Siagi ya karanga ina kalori nyingi zitakazokuwezesha ubaki ni mwenye nguvu kutwa nzima.

  1. chumvi ya mawe

Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijasafishwa au haijapita kiwandani ina mchango mkubwa sana katika kutibu tatizo hili. Tumia chumvi hii kwenye vyakula vyako kila siku.

  1. Spinachi

Folic asidi ni kitu mhimu katika kuongezeka kwa mbegu za kiume. Spinachi na mboga nyingine za majani zenye rangi ya kijani ni mhimu kwa ajili hii sababu ya vitamini na kuweka sawa usawa wa ‘folate’ kwenye mfumo wako wa mwili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags