Harmonize: Nilikuwa sina pa kulala nilivyoachana na Sarah

Harmonize: Nilikuwa sina pa kulala nilivyoachana na Sarah

Eeeeeheee! Kumekucha pande hizi umakondeni bwana baada ya aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Konde boy jana kuonekana mahakamani kwenda kudai talaka na kugawana mali na Harmonize.

Basi bwana Kupitia InstaStory ya Harmonize ame-share chats zake na mchumba wake wa sasa Kajala kuhusu jinsi alivyokosa pa kulala baada ya kuachana na Sarah.

Ambapo chats hizo zikiwa zimeandikwa, “tumeachana nikaanza kulala nyumbani kwako daah hata pa kulala nilikuwa sina, hizo mali zilikuwa wapi jamani,” ameandika Harmonize.

Haya haya wale wenzangu na mie embu kujeni hapa ni kweli Konde Boy alikuwa analala kwa Kajala au tumepigwa na kitu kizito? Dondosheni koment hapo chini

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags