Haji Manara na Dulla Makabila kwenye bifu zito

Haji Manara na Dulla Makabila kwenye bifu zito

Zikiwa zimepita siku mbili tangu aliyekuwa mke wa Mwanamuziki wa singeli nchini Dulla Makabila, Zaylissa kuvishwa pete Januari 18 na aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara, kumezuka gumzo mitandaoni baada ya Makabila kuachia wimbo uitwao 'Furahi'.

Wimbo huo unadaiwa kuwa Makabila amemuimbia Zaylissa kutokana na mistari yake inavyosikika, baada ya kuachiwa rasmi jana Jioni, Makabila amedai kupokea jumbe za vitisho kutoka kwa Manara, zilizoandikwa.

“Umeanza mimi nakuja kumaliza hii video yako ya kujiliza itakuwa gumzo na usije kunilaumu na ninazo kumi na SMS zako umemchokoza gwiji wa hizi kazi usije baadaye kutafuta huruma.

"Umemtukana na kutaka kumdhalilisha mtu mwenye silaha zako kibao na akakuhifadhi siku zote sasa kwa kuwa unataka kiki na trending utaipata hasa, usiku mwema na jiandae kisaikolojia.” Ameandika Manara.

Kufuatiwa meseji hizo hivyo Makabila hakulikalia kimya suala hilo ambapo alirudisha mashambulizi kwa ku-post picha ya Haji Manara ikiwa imeambatana na ujumbe ukieleza kuwa anataka Manara 'asapoti' wimbo wake kwani siku zote huwa wa kwanza kufanya hivyo.

Hadi sasa wimbo huo wa Dulla unashika namba moja kusikilizwa kwenye mtandao wa YouTube, huku ukiwa na watazamaji zaidi ya laki mbili. Ikumbukwe Makabila na Zaylissa walifunga ndoa Mei 2023 na kuachana Julai mwaka huohuo, hivyo basi ndoa yao ilidumu kwa mwezi mmoja tuu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags