Fahamu vitu vinavyoweza kuimarisha tendo la ndoa

Fahamu vitu vinavyoweza kuimarisha tendo la ndoa

Kila mtu ana stori ya namna yake inayohusu mapenzi hususani katika swala la tendo la ndoa, pia imekuwa changamoto na hata chanzo cha kutengana kwa baadhi ya wana ndoa na wapendano (wachumba).

Katika mitandao ya kijamii kulikuwa na mjadala mrefu na kila mtu akisema mtazamo wake baada ya hotuba ya Rais mama Samia kuhusiana na swala la vijana kutumia supu ya pweza na mkongo ili kujiridhisha katika tendo la ndoa, basi mwanao wa faida nikaamua kuingia mtaani kuzungumza na wadau mbalimbali ili kujua vitu au vyakula ambavyo vinaweza kuimarisha tendo la ndoa. Je unajua ni vyakula gani? Je supu ya pweza ina umuhimu gani?

Kama kungekuwa na ushahidi kwamba chakula cha aina moja kinaweza kuimarisha tendo la ndoa na kukuzidishia hamu, huenda kungekuwa na uhaba wa chakula hicho lakini ukweli usiofichika ni kwamba uimara wa tendo hutegemea zaidi lishe bora, kufanya mazoezi na afya nzuri ya akili.

 

  • Miongoni mwa vyakula  vinavyoweza kukuongezea hamu ya tendo ni pamoja na vitoweo kutoka baharini yani chaza na pweza.

Chaza na pweza wana virutubisho vinavyoweza kuchochea hisia ya furaha kutokana na homoni ya endorphins. Virutubisho hivyo vinahusishwa na kuimarika kwa tendo la ndoa kwani chaza ana asili ya madini ya zinc yenye kirutubisho muhimu kinachotumika kuunda homoni ya testosterone.

Wataalamu wa afya ya uzazi wanasema  kwamba madini ya zinc yanaweza kusaidia na kutibu matatizo ya wanaume kuweza kuzalisha na kuongeza ubora wa manii, pia vyanzo vingine vizuri vya madini ya zinc hupatikana katika nyama nyekundu, mbegu kama za tango, korosho, maziwa na jibini. 
 

  • Ulaji wa Chokoleti

Kula chokoleti nyeusi kunaweza kukupa hisia ya awali unapompenda mtu, kwa sababu ina  'kemikali ya mapenzi' phenylethylamine (PEA).

PEA - ambayo huwepo katika miezi ya kwanza ya mahusiano ambayo huchangia kuwepo kwa homoni inayomfanya mtu kujihisi vizuri na kuchochea raha katikati mwa ubongo.

Kemikali ya PEA inapatikana kwa kiwango kidogo katika chokoleti na kiwango hicho kinaendelea kuwepo wakati kinaliwa, vilevile cocoa husaidia kuimarisha tendo la ndoa kwani ina amino acid tryptophan, ambayo huongeza msukumo wa damu na viwango vya serotonin (homoni nyingine ya furaha).

  • Pilipili zina kinachojulikana kama capsaicin

Wataalamu wanasema pilipili inaweza kuchochea homoni ya endorphins ambayo husababisha mtu kujihisi furaha.

Pia pilipili husaidia uharakishaji au ufanyaji kazi mfumo wa kusaga chakula tumboni na huongeza ujoto mwilini na kasi ya moyo unavyopiga.

Lakini hakikisha kwamba unakumbuka kuosha mkono unapotayarisha pilipili!

Hivyo ndo baadhi ya vitu au vyakula ninavyoweza kuimarisha tendo la ndoa kwa mujibu wa taalamu.

Kwa story nyingine zaidi, usiache kutembelea kurasa zetu za Mwananchi Scoop uweze kujifunza zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post

Latest Tags