FAHAMU KWA UNDANI UGONJWA WA WASIWASI

FAHAMU KWA UNDANI UGONJWA WA WASIWASI

Unaweza kujiuliza wasiwasi nao ni ugonjwa eti?

Kisaikolojia huu ni ugonjwa ambao unasumbua baadhi ya watu na kwa sasa umekuwa mkubwa kutoka na mambo ya sayansi na tekelojia.

Wasiwasi maana yake ni hisia ya kutotulia au hofu apatayo mtu katika vipindi mbalimbali lakini pia ni majibu ya asili ya mwili wako kwa mafadhaiko.

Kwa mfano siku ya kwanza ya shule au chuo wengi hupata wasiwasi kwa sababu ya mazingira ambayo ni mageni kwake au   kwenda kwenye mahojiano ya kazi, au kutoa hotuba inaweza kusababisha watu wengi kupa hofu na woga.

kisaikolojia hii ni hali ya kawaida kwa mwanadamu yoyote, lakini ikiwa hisia zako za wasiwasi ni kali, hudumu kwa zaidi ya miezi sita, na zinaingilia maisha yako, hivyo itakufanya uanze kupata msaaada wa kisaikolojia.

Dalili za ugonjwa huu

-Kuwa na hofu ya mara kwa mara

-Kukosa usingizi

-Midomo kukauka

-Misuli kukaza

-Kukosa utulivu

 

-Ongezeko la mapigo ya moyo

 

Tiba ya ugonjwa huu

Kama maisha yako si ya furaha sana ni ya msongo wa mawazo kila wakati ni rahisi sana kuwa na wasiwasi.

Hivyo basi jaribu kufanya yafuatayo yatakupunguzia kuwa na wasiwasi na kudhibiti kupata dalili za kuwa na ugonjwa huo uliozidi.

Kwanza jichanganye na wengine, Upweke unaweza kukuletea au kukuongezea wasiwasi, jaribu kuyazungumzia ana kwa ana matatizo yako ya kuwa na wasiwasi itakusaidia kuupunguza wasiwasi uliokuwa nao.

Jitahidi kila wakati kukutana na marafiki zako pia jaribu kuwashirikisha mambo yanayokusumbua mtu umpendaye.

Pia jitahidi kujiepusha na mambo ambayo yanakuleta msongo wa mawazo. Unaweza kuonana na wanasaikolojia ambao watakusaidia kupungua msongo wa mawazo.

Vilevile pendelea kufikiria mambo chaya zaidi kuliko hasi hii itakusaidia kupona wasiwasi.

Aidha jenga tabia ya kufanya mazoezi hasa ya kulegeza misuli, kuvuta pumzi kwa nguvu, hizi ni njia ya asili ya kupunguza wasiwasi na msongo wa mawazo pia.

kupata matokeo bora kabisa jenga tabia ya kufanya mazoezi ya kuongeza mapingo ya moyo na kutoka jasho kwa muda wa dakika 30 kila siku.

Mazoezi au shughuli za kuifanya mikono na miguu kuwa katika mwendo kwa wakati mmoja ni ya manufaa sana, jaribu kutembea, kukimbia, kuogelea, kucheza muziki wa dansi.

Pata usingizi wa kutosha kwani kukosa usingizi kunaweza kukuza tatizo la kuwa na wasiwasi kwa hivyo binadamu yoyote anatakiwa kulala masaa 8 ya usingizi. jitahidi kupata usingizi kama imeshindikana kupata usingizi onana na wataalamu watakupatia dawa jitakusaidia kupata usingizi.

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags