Fahamu jinsi ya Kumlisha Mtoto Maziwa ya Kopo

Fahamu jinsi ya Kumlisha Mtoto Maziwa ya Kopo

Kuna aina nyingi za maziwa ya unga yaliyotengenezwa maalumu kwa watoto wachanga.

Mratibu wa lishe Manispaa ya Temeke, Dk Charles Malale ndani ya jarida la MwananchiScoop leo anafunguka juu ya namna bora ya kumlisha mtoto maziwa ya kopo.

Dk. Malale anasema ili kuweza kumlisha kwa usahihi mtoto maziwa ya kopo, mzazi anapaswa kila mara kuhakikisha anatumia maziwa yaliyotengenezwa maalumu kwa watoto wachanga.

Anasema pia ni muhimu mama kila wakati kukumbuka kusoma na kufuata kwa makini maelekezo kwenye kopo la maziwa atakalonunua.

“Ni vema sana kutengeneza maziwa ya kutosha kwa mlo mmoja ukifuata maelekezo yanayotolewa, pia hakikisha una maziwa ya kutosha kumtayarishia mtoto kila siku,” anasema Dk. Malale

Anasema watoto huhitaji maziwa ya kopo mengi zaidi kadiri wanavyokua ambapo kwa miezi sita ya mwanzo, mtoto atahitaji kati ya makopo 40 na 51 ya maziwa kutegemea uzito wa kopo (400g-500g).

Jinsi ya kutayarisha maziwa ya kopo

Anasema kila mara mtayarishaji anapaswa kuhakikisha anatumia maziwa ya kopo yaliyotengenezwa maalumu kwa watoto wachanga.

Dk. Malale anasema mtayarishaji anatakiwa kuwa na maji safi na salama ya kuchanganya na maziwa ya kopo, kama anaweza basi achemshe maji atakayohitaji kwa siku nzima.

“Kila mara osha vyombo unavyotumia kutayarisha maziwa ya kopo na kumlisha mtoto kama vikombe, vipima ujazo, vijiko na vyombo vingine kwa maji safi na sabuni,” anasema

Anasema ni vema zaidi kuchemsha vyombo kila mara ili kuhakikisha ni safi na salama.

“Kila mara unapaswa kunawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka kabla ya kutayarisha maziwa ya kopo na kumlisha mtoto,” anasema na kuongeza

“Tayrisha vyombo vyote utkvyohitaji kutumia kupima ujazo, tumia kijiko maalumu kilichpndani ya kopo la maziwa ya watoto kupima kiasi cha maziwa,” anasema

Changanya maziwa ya mtoto kwa makini

Anasema wakati wote mama anapaswa kufuata maelekezo yaliyo kwenye kopo la mazima kwa kutumia kijiko maalumu kilichopo ndani ya kopo kwa ujazo mfuto.

“Weka maziwa hayo kwenye chombo kilichowekwa alama, idadi ya vijiko vya maziwa utakavyotumia hutegemea umri wa mtoto, weka kiasi kidogo cha maji yaliyochemshwa na kupoa kwenye kikombe chenye maziwa na kukoroga kuxuia mabonge,” anasema

Anasema kwa kuzingatia maelekezo kwenye kopo, wakati wa kuchanganya maziwa mtayarishaji atatakiwa kuongeza maji ya moto mpaka kwenye alama iliyowekwa, kuzidisha u kuweka kiasi kidogo cha maji huweza kuhatarisha afya ya mtoto.

Nitamlishaje mtoto?

Dk. Malale anasema kila mara mama au mlezi anapaswa kumlisha mtoto kwa kutumia kikombe safi kilichowazi.

“Hata mtoto mchanga hujifunza haraka kunywa kwa kikombe, epuka kutumia chupa na chuchu kwa vile ni vigumu kusafisha pia huweza kumsababishia mtoto maradhi,” anasema

Anasema kama mtoto hatamaliza maziwa yote yaliyotayarishwa, yatakayobaki yatumike kwa chakula cha familia na kuongeza kuwa ni muhimu kuepuka kumpa mtoto maziwa yaliyobakia kwani huweza kusababisha maradhi.

Kumbuka

Anasema wanawake wanaoishi na VVU hawapaswi kunyonyesha maziwa yao baada ya kuwapa watoto maziwa ya kopo kwani ulishaji huo huongeza uwezekano a maambukizi ya VVU kwa mtoto.

Dk. Malale pia anasema iwapo mtu ataishiwa maziwa ya kopo, asimnyonyoshe wala asitumie maji mengi zaidi kwa kuchanganya na maziwa ya kopo ili yawe mengi, badala yake amlishe mtoto maziwa mabichi ya ng’ombe yaliyorekebishwa kwa maji, sukari na mikronutrienti mpaka yatakapopatikana mazima mengine ya kopo.

“Pia mtoto atahitaji kupewa maziwa ya kopo tu kwa kipindi cha miezi 6 ya mwanzo, bila kumpa chakula, maji au kinywaji kingine chochote. Mtoto akitimiza miezi 6 endelea kumpa maziwa ya kopo au maziwa ya ng’ombe yasiyoongezwa naji ba anza kumpa chakula cha nyongeza kilichosafi na chenye virutubishi.

“Iwapo una maswali yanayohusu ulishaji wa mtoto wako, mwone mnasihi upate msaada, kuwa makini na dalili za kuhara, homa, kupumua kwa shida au kukataa chakula. Unapogundua moja ya dalili hizi mpeleke mtoto katika kituo cha afya haraka,” anasema

Aidha anasema wanawake wasionyonyesha watoto wao wanaweza kupata mimba mapema kuliko wale wanaonyonyesha, huku akisisitiza ili kulinda afya ni muhimu kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu kila mara kwa usahihi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags