Eric Omondi : amapiano imeua muziki wa bongo fleva

Eric Omondi : amapiano imeua muziki wa bongo fleva

Moja ya story ambazo zinaendelea kuleta gumzo katika mitandao ya kijamii ni hii ya mchekeshaji kutokea pande za Kenya, Erick Omondi ambaye amefunguka na kusema Amapiano imeua muziki wa BongoFlava.

Aisee unaambiwa kauli hiyo imeungwa mkono na wadau mbalimbali hasa mashabiki wa muziki wa Tanzania na kusema wasanii wanapaswa kubadilika na kuachana na Amapiano.

Hata hivyo Mchekeshaji huyo amesema kwa Afrika Mashariki msanii Diamond Platnumz ndio anayemtambua na anastahili kupewa sifa hizo.

Kupitia post yake ya Instagram inasema kuwa wasanii wa Kenya wamelala, Tanzania wamepoteza kwenye Amapiano, na Uganda wameacha kuimba hawajaribu tena.

"Wizkid alijaza 02 Arena siku 3 na Chris Brown alikuwepo, Burna Boy anashinda Grammys kila mwaka, Kenya wanaowasilisha kwenye Michezo ya Olimpiki ya muziki wa Kiafrika na mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye miaka 14".

"Mwanamuziki Pekee wa Afrika Mashariki ninayemkubali ni Diamond Platnumz (Tumpe sifa pale anapostahili Chibu anajaribu), Sauti sol wanajaribu lakini haitoshi" amesema Omondi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags