Dua, sala zamimimka kumuombea Professor Jay

Dua, sala zamimimka kumuombea Professor Jay

 

 

Moja ya kitu kikubwa kinachofanywa na mastaa mbalimbali hapa nchini ni kumuombea dua na sala za kumtakia afya njema mkongwe wa Hip Hop Bongo, Joseph Haule almaarufu Professor Jay ili iendelee kuimarika.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba hali yake kiafya si nzuri na kwamba amelazwa kwenye moja ya hospitali kubwa jijini Dar.

Miongoni mwa mastaa waliompa pole na kumtakia afya njema Professor Jay ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Mikumi ni Diamond Platnumz aliyemuandikia; “Get well soon prof…”

Staa mwingine ni Shilole ambaye katika ukurasa wake wa Instagram aliandika "Upo kwenye maombi kaka yangu kutoka moyoni mwangu na hakuna linaloshindikana mbele ya Mungu ugua pole na upone urudi kwenye mishe zako,"

Itakumbukwa January 28, mwaka huu, mtu wa karibu na msanii huyo, Don Colean255 alifunguka juu ya afya ya Professor Jay

Don Colean255 ni mtu wa karibu na Professor Jay ambaye alisema hali ya msanii huyo bado si nzuri na kwa sasa yupo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akiendelea na matibabu.

Rafiki huyo alisema tangu Jumatatu ya Februari 24, mwaka huu Professor Jay hali yake ilibadilika na kupelekwa hospitali ya Lugalo ambayo baada ya kumpima walimuhamishia Muhimbili kutokana na hali yake kutokuwa nzuri

MwananchiScoop tnaungana na wote wanaomuombea Professor Jay apone haraka ili aendelee kutoka burudani kwa mashabiki wake.

Professor Jay ni mmoja wa waasisi wa muziki wa Kizazi Kipya nchini ambao kwa sasa unaajiri vijana wengi na kuwapa mkate wa kila siku.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags