Aidha katika sherehe hiyo ya mwisho iliyofanyika Jamuhuri ya Dominica baadhi ya ndugu na jamaa wametoa maoni yao kuhusu marehemu huyo wakieleza kuwa alikuwa ni mtu mwema.
Hata hivyo Binti wa mwanamuziki huyo Zulinka Perez ambaye pia alikuwepo katika ukumbi huo na baba yake amefunguka kuwa anabahati ya kuendelea kuwa hai.

“Mimi na mume wangu ni mashahidi wa muujiza kwasababu tulikuwa kando yake.Sisi nimanusura wa mkasa huo.Nilikiona kilichojiri pale,hakuna atakayenisimulia.Namshukuru Mungu na mume wangu niko hai kwasababu alinifunika na mwili wake na ndiyo maana niko hapa,” amesema Zulinka.
Ikumbukwe msanii huyo na mashabiki wamefariki wakati wa tamasha la "Merengue Monday" ambalo lilifanyika katika klabu ya usiku iitwayo ‘Jet Set’ mapema wiki hii.
Mamlaka bado haijabaini sababu ya kuporomoka kwa paa hilo huku idadi ya waliopoteza maisha ikifikia 218 na watu zaidi ya 189 waliokolewa wakiwa hai wengine wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali nchini humo.
Leave a Reply