Inaelezwa kuwa kijana huyo alichukua uamuzi huo baada ya kutendwa kwa muda mrefu katika mahusiano yake huku akidai kuwa toka aanze kujiingiza kwenye mahusiano hajawahi kuacha badala yake amekuwa akiachwa mara kwa mara.
Ripoti zinasema kuwa alimuoa mbuzi, akidai kuwa ni mtiifu, mtulivu, na wala hatomsaliti kama ambavyo wamekuwa wakifanya wapenzi wake wa nyuma.

Geo si mwanaume wa kwanza kuchukua uamuzi wa kufunga ndoa na Mbuzi kwani miaka ya nyuma kuliwahi kutokea matukio kama hayo, mwanaume mmoja aitwaye Bhagwan Singh, mwenye umri wa miaka 27 kutoka jimbo la Madhya Pradesh, aliamua kumuoa mbuzi wake baada ya kupitia matatizo ya mapenzi.
Lakini pia mwanaume mwingine aitwaye Saiful Arif kutoka Indonesia alimuoa mbuzi kwa nia ya kuvutia watu kwenye mitandao ya kijamii, huku mahari ya rupiah 22,000 ikitolewa.
Leave a Reply