Kwa mujibu wa Glenn Gordon Caron mwanzishi wa kipindi cha ‘Moonlighting’ ambacho alikuwa akifanya na Bruce amefunguka kuwa hali ya mwigizaji huyo inazidi kuwa mbaya kwani kwasasa amepoteza kabisa uwezo wa kuwasiliana na watu.
“Sasa hawezi kuzungumza vizuri, hawezi kuwasiliana kabisa, sio mzungumzaji tena na kama atazungumza basi kwa asilimia moja ugonjwa wake umemfanya kuwa mkimya sana,”amesema Glenn
Japokuwa hali yake imezidi kuwa mbaya, familia yake bado iko karibu naye, ikijaribu kuweka mazingira ya upendo na faraja. Mke wake, Emma Heming Willis, amekuwa mstari wa mbele kutoa elimu na kuhamasisha watu kuhusu FTD, akisisitiza kwamba licha ya ugonjwa huo, bado kuna njia za kufurahia maisha na kuweka uhusiano wa kihisia na wapendwa.

Bruce aligundulika kuwa na Frontotemporal Dementia (FTD), mwaka 2022 aina ya ugonjwa wa akili unaoathiri sehemu za ubongo zinazohusika na lugha, tabia, na mawasiliano pamoja na kumbukumbu.
Alitambulika zaidi kupitia filamu kama Pulp Fiction, The Fifth Element, The Sixth Sense, na Unbreakable huku filamu yake ya mwisho kucheza ikiwa ni ‘Assassin’ iliyotoka mwaka 2023.
Leave a Reply