Drake, Taylar, Adele, Tupac, Bieber ndiyo basi tena tiktok

Drake, Taylar, Adele, Tupac, Bieber ndiyo basi tena tiktok

Shirika la ‘Universal Music Group’ linalojihusisha na masuala ya haki milizi za wasanii limeamua kuondoa nyimbo zake katika mtandao wa kijamii wa TikTok baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya haki miliki.

Uamuzi huo umekuja baada ya wamiliki wa Tiktok na Universal Music Group kutofikia makubaliano katika kikao kilichokaliwa siku ya jana Januari 30, ambapo ilibainika kuwa mtandao wa Tiktok umekuwa ukitoa kiasi kidogo cha mirabaha licha ya mtandao huo kuwa na zaidi ya watumiaji bilioni moja.

Mkataba waliosaini miaka mitatu iliyopita utatamatika siku ya leo Januari 31, hivyo basi kuanzia kesho Februari 1, nyimbo zote zenye haki miliki ya Universal hazitapatikana katika mtandao wa TikTok.

TikTok imeeleza kuwa itaendelea ku-support wasanii na ‘lebo’ nyingine ambazo zinaelewa na kufuata makubaliano ya haki miliki.

Wasanii maarufu ambao Universal wanahaki miliki za ngoma zao ni Justin Bieber, Drake, The Weeknd, Taylor Swift, Adele, Billie Eilish, post Malone, Ice Spice, TuPac, Nicki Minaj, SZA, Alicia Keys, Bad Bunny, Kendrick Lamar na wengineo.
.
.
.
#MwannchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags